22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Halmashauri zatakiwa kujenga masoko yakupokea mazao ya wakulima

Safina Sarwatt, Moshi

Halmashauri nchini zimezitakiwa kujenga masoko maalum yatakayo pokea mazao ya wakulima na kuyapima kwa kilo ili kukomesha vipimo vya rumbesa vinavyotumika kuwaibia wakulima kipindi wanapovuna mazao yao.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Machi 17, 2021 na Kaimu Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Kilimanjaro Dennis Misango, wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake juu ya malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na wakulima kulazimika kuuza mazao yao kwa mtindo wa rumbesa.

Misango amesema ili kukomesha wakulima wasiendelee kuwalanguliwa mazao yao na wafanyabiashara mashambani kila Halmashauri haina budi kujenga vituo na masoko maalum ambayo yatakuwa na mizani sahihi za kupimia mazao ya wakulima kila wanapotaka kuyauza mazao yao.

“Tumejipanga kukomesha vipimo vinavyoitwa Shishimbi kwa mazao ya vitunguu na karoti na viazi ambapo kipimo hiki gania moja linakuwa na kilo 165 hadi 170 huku kipimo kinachojulikana kwa jina la Kenya gunia moja linakuwa na kilo 150 hadi kilo 165 na tunatakiwa tubaki na kipimo kinachoitwa Magufuli ambapo gunia moja linakuwa na kilo 95 hadi 100,”amesema Misango.

Amesema wakala wa vipimo mkoani hapa imejipanga kuhakikisha inawakamata wafanyabiashaea wote wanaotumia mizani mibovu kwani sheria ipo wazi kwa mfanyabiashara atakayekamatwa na kukiri kosa lake faini yake ni kuanzia shilingi 100,000 hadi Sh milioni 20.

Amesema sheria, kanuni na mwongozo wa Werikali wa Wakala wa Vipimo inaelekeza mazao yote ya wakulima yatafungashwa kwa uzito wa kilo mia moja na si vinginevyo na endapo mkulima atatumia vipimo vingine atakuwa ametumia vipimo batili na kuibiwa.

Ameongeza kuwa Serikali imepiga marufuku vipimo vya kutumia madebe, ndoo, sadolini na makopo yaliyopondwa vinavyotumika katika masoko mbali mbali kwani vipimo hivyo ni batili na vinawaibia wananchi .

Amesema wakulima walio wengi bado wanakabiliwa na changamoto ya kulanguliwa mazao yao mashambani na wafanyabiashara ambao wamekuwa wakienda moja kwa moja mashambani na kununua mazao hayo kwa makadirio bila kuwa na mizani jambo ambalo limeendelea kuwaumiza wakulima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles