25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wanawake washauriwa kula vyakula vyenye madiniya folic Acid

Na Tunu Nassoro, Dar es Salaam

Wasichana  ambao bado hawajazaa na wanawake walio kwenye umri wa kuzaa wameshauriwa kula vyakula vyenye madini ya folic acid zikiwamo mboga za majani na matunda ili kuwaepusha na matatizo ya kuzaa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Akizungumza katika semina ya waandishi wa habari Machi 12, 2021 Ofisa Maendeleo wa Chama cha Wazazi wa watoto wenye Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (Asbaht), Theresia Jacob, amesema tatizo hilo linazidi kuwa kubwa kutokana na wasichana kula vyakula visivyo na virutubisho.

“Kwa utafiti nilioufaya katika vyuo vitatu nimebaini kuwa asilmiia kubwa ya wasichana ambao wanatarajiwa kuwa wazazi wa baadaye hula Chips na kuku katika milo yao bila kuongeza mboga za majani na matunda,” amesema Theresia.

Amesema kwa sasa hospitali ya Tiba ya mifupa na mishipa ya fahamu (MOI) hupokea watoto kati ya watano hadi sita kwa wiki jambo ambalo linaonesha tatizo hilo kukita mizizi katika jamii.

“Tulichokibaini mikoa inayolima matunda ya biashara wanawake wamekuwa hawakumbuki kula matunda hayo badala yake huyauza yote,” amesema Theresia.

Naye daktari bngwa wa upasuaji, Dk Consolatha Shayo ameitaka jamii kutokuwaficha watoto hao bali wawawahishe hospitali kupata matibabu.

“Tunashauri wasichana na wanawake wanaotarajia kubeba ujauzito kuanza kunywa dawa za ‘folic acid’ miezi mitatu kabla ya kubeba ujauzito na kuendelea kunywa katika kipindi cha ujauzito na mpaka atakapojifungua ili kuepuka tatizo la kichwa kikubwa na mgongo wazi,” amesema Dk. Consolatha.

Baadhi ya kina mama ambao ndio walezi wa watoto wenye matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi wamesema  wanakabiliwa na tatizo la unyanyapaa katika jamii huku miongoni mwao wakikiri hata kuvunjika kwa ndoa zao baada ya kujifungua watoto wenye matatizo hayo.

Mmoja wa wanawake hao Ramla Makame Juma amesema kumekuwa na dhana potofu kwa jamii kuwa kupata mtoto mwenye tatizo hilo ni ushirikina jambo lnaloongeza unyapaa katika jamii.

Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa, Katibwa Afya Mkoa wa Dar es Salaaam Sister Mathew amesema serikali ya mkoa inahakikisha dawa za folic acid zinapatikana katika vituo vyote vya afya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles