26.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 16, 2024

Contact us: [email protected]

Hall: Uzembe utaigharimu timu

hallNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall, amesema uzembe ambao umekuwa ukifanywa na wachezaji wake mara kwa mara utapelekea timu hiyo kushindwa kutimiza malengo waliyojiwekea mwaka huu.

Azam, ambayo itashuka dimbani Jumapili kuvaana na Esperance ya Tunisia katika michuano ya Kombe la Shirikisho, iliambulia sare ya mabao 2-2 kutoka kwa Ndanda FC, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa juzi Uwanja wa Azam Complex.

Habari za ndani kutoka kwa mmoja wa viongozi wa klabu hiyo zilidai kuwa mara kwa mara wachezaji wamekuwa wakirudia makosa ambayo Kocha Hall amekuwa akiyafanyia marekebisho.

“Tumepoteza mchezo huu, kocha amelalamika kweli na amedai uzembe wa makusudi umekuwa ukifanywa na wachezaji wetu, jambo ambalo litatugharimu huko mbele,” alisema.

Alisema, Hall amejiwekea malengo ya kuifikisha mbali timu hiyo katika michuano ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho, kama wachezaji watakuwa wakionyesha makosa ya wazi kila wakati hakuna watakachovuna.

“Unadhani kama tunashindwa kuonyesha umakini kwenye mechi za ligi, hiyo michuano ya kimataifa ambayo ni migumu itakuwaje, tutaambulia ziro kabisa.

“Wachezaji wamekuwa wakifanya utoto, wanajitahidi dakika chache baada ya hapo wanaishia kuboronga na kujisahau kabisa, hali hiyo imekuwa ikirudisha nyuma malengo ya mwalimu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles