27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Hakielimu yafundisha wanafunzi kutengeneza taulo za kike za kienyeji

NA FLORENCE SANAWA- MASASI


TAASISI ya HakiElimu imeanza kutoa elimu ya kutengeneza taulo za kike za asili kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Tayari taasisi hiyo imetoa mafunzo hayo kwenye shule za wilaya 11 zikiwamo shule za msingi na sekondari    wilayani Masasi.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Ofisa Programu wa  shirika hilo, Alinanuswe Kasyele, alisema wamedhamiria kumsadiai mtoto wa kike  kupunguza utoro shuleni wakati wa hedhi.

Alisema taasisi hiyo inatarajia kufika katika halmashauri 22 na katika kila halmashauri wamechagua shule mbili za sekondari na msingi.

Alisema wanafunzi wengi wa kike wamekuwa wakiachwa nyuma katika elimu.

Kasyele alisema kwa sababu hiyo taasisi hiyo  imeanzisha  mpango mkakati wa kuwawezesha   kufurahia vipindi darasani wakati wakiwa katika siku zao za hedhi.

“Wanafunzi wa kike wana changamoto mbalimbali lakini tunaona kuwa kitendo cha wanafunzi kukosa masomo kwa siku tatu hadi tano inachangia ufaulu hafifu kwa wanafunzi wa kike nchini.

“Ndiyo maana tulikuja na huu utaratibu ambao kwa njia rahisi wanaweza kutengeneza taulo za kike na wakazitumia kwa muda mrefu zaidi na kupunguza gharama,” alisema.

Kaimu Ofisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Luth Tunzo, alisema usafi ni wa msingi kwa mwanamke hasa anapokuwa kwenye hedhi.

“Unajua wazazi wengi vijijini hawana uwezo wa kununua pedi ndiyo maana tunaamini kuwa mafunzo ya kutengeneza hizi   pedi yataokoa gharama kwa wazazi wengi,” alisema.

Msimamizi wa klabu za ulinzi wa mtoto katika mradi wa The Girls Retention and Transition Initiative (GRTI), Blandina Nakajumo, alisema wakati wa hedhi wanafunzi wengi wa kike hushindwa kufika shuleni.

Alisema kitendo hicho kimefanya shirika hilo kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa kike  waweze kujua kutengeneza pedi kwa njia rahisi zaidi isiyo na gharama kubwa.

“Jambo hili tunapaswa kuwashirikisha wanajamii wote wanawake kwa wanaume   kuwasaidia watoto wa kike wasipoteze muda wao na kushindwa kuhudhuria darasani.

“Tutafurahi zaidi wanaume wakiwa chachu ya maendeleo kwa mtoto wa kike,” alisema Nakajumo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles