26.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

HABBAT SODA: MAFUTA YANAYOTIBU MAGONJWA 89

Habbat Soda

INAPOTOKEA wafalme wa Misri, Malkia wa Ulaya, Mitume na wanasayansi wa kisasa wanakuja na kukubaliana katika jambo moja, ni muhimu kudadisi juu ya jambo hilo. Ingawa nyakati za sasa tunazungukwa na taarifa na elimu nyingi kuliko katika wakati mwingine wowote, bado tunahitaji kujifunza vitu kutokana na historia na maisha ya kale.

Kutoka kwa baba wa sayansi ya matibabu katika nchi za magharibi Hippocrates kwenda mpaka kwa kiongozi wa mfumo wa mwisho wa kifarao Cleopatra hadi kwa mfalme Tut na jamii iliyofuata, kitu cha pekee ambacho walikuwa wakifanana viongozi hawa kwa pamoja ilikuwa ni thamani waliyoiona katika mtishamba fulani.

Mtishamba au mmea huo ambao viongozi hao walikutana pamoja si mwingine bali ni habbat soda. Habbat soda ndilo jina linalotumika zaidi mashariki ya kati na huko ulaya huitwa ‘black seeds’.

Kwahiyo, niliamua kuchukua muda kusoma na kupeleleza zaidi kuhusu habbat soda kwa faida yangu na ya wasomaji ili hatimaye niweze kukuletea mwanga kamili juu ya mengi yanayosemwa kuhusu mafuta ya  habbat soda.

Unaweza kuwa umesikia majina tofauti tofauti ya habbat soda kutegemea na sehemu gani ya dunia ulipo.

Haya ni moja ya majina yake

Kalonji Oil, Black Cumin Seed Oil, Nigella Seeds, Graine De Nigelle, Black Onion Seeds na Schwarzkummel. 

Asili yake

Mafuta ya habbat soda yanatokana na mbegu za habbat soda na mbegu hizi huwa ni nyeusi na ndiyo maana kwa Kiingereza wanaita ‘black seed’. Kuna mashine nyingi za nyumbani unazoweza kutumia kutengeneza mafuta yako mwenyewe kutoka katika mbegu za habbat soda ingawa bado unashauri ununuwe yale ambayo yameandaliwa tayari.

 Sifa zake

Huondoa bakteria mwilini, uvimbe, sumu na fangasi. Pia inatibu saratani, pumu, inadhibiti kazi za histamini, inaua virusi na kuzuia damu kuganda.

Vitu viwili muhimu zaidi ambavyo mafuta haya yanavyo ni ‘thymoquinone’ na ‘thymohydroquinone’.

Vimeng’enya hivi viwili ndivyo vinaweza kusemwa kuwa ndiyo sababu ya mafuta haya kuwa ni dawa kwa magonjwa mengi. Vinaimarisha moja kwa moja kinga yako ya mwili na kuifanya ipatikane wakati wowote itakapohitajika na mwili. 

Mbegu za habbat soda

Mbegu za habbat soda zinatoka katika majani ya mmea wa ‘Nigella Sativa’ na unalimwa karibu katika kila pembe ya dunia kwa sasa. Asili yake ni Afrika kaskazini, mediterania/Ulaya na Asia na kutoka hapo umesambaa kila sehemu ya dunia. Habbat soda inachukuliwa kama moja ya dawa za asili bora zaidi kuwahi kutokea.

Yanavyofanya kazi mwilini
Kuna matumizi mengi ya habbat soda katika kutibu na kukinga magonjwa mbalimbali. Hapa nimejaribu kukusanya baadhi ya magonjwa 89 ambayo unaweza kujitibu kwa kutumia mafuta haya. 

Majani ya habbat soda

Habbat soda kwa kawaida husaidia magonjwa yafuatayo: 

  1. Kuimarisha afya ya moyo

Afya mbovu ya moyo inaweza kuwa ni matokeo ya sababu nyingi lakini sababu zote chanzo chake kikuu ni matokeo ya kutokuupa moyo virutubishi unavyovihitaji.

Mafuta ya habbat soda yana asidi mafuta safi na yenye Omega 6 na 9, pia yana kirutubishi kingine muhimu zaidi cha ‘phytosterols’ ambacho husaidia kulazimisha kusinyaa na kutanuka kwa mishipa ya damu na hivyo kusaidia kuzuia damu kuganda na kujikaza katika ateri.

Viinilishe hivi pia husaidia kushusha lehemu kwenye damu na kiasi cha damu sukari.

Kwa karne nyingi mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika kutibu matatizo mengi yanayohusiana na moyo.

  1. Hupigana na maambukizi ya fangasi

Maambukizi ya fangasi yanatokea wakati bakteria wanapozidi juu ya ngozi yako na kusababisha kutokea kwa magonjwa mengi ikiwamo miwasho, upele na ukurutu. Tafiti zinaonyesha kuwa mafuta ya habbat soda ni mazuri kwa tiba karibu kwa kila aina ya fangasi kitu kinachowafanya wanasayansi wengi kuamini kuwa habbat soda ni dawa ya asili na mbadala muhimu zaidi kwa kila mtu kuwa nayo nyumbani. 

  1. Hudhibiti Aleji (mzio)

Wengi wetu tunapatwa na aleji na kutokewa na chafya au mafua yasiyoisha hivyo kusababisha kushuka kwa kinga ya mwili. Kutumia mafuta asili ya habbat soda kwa ajili ya kutibu aleji kunaweza kuleta matokeo mazuri bila gharama kubwa. Si kwamba mafuta haya yatakupa nafuu kwa haraka dhidi ya aleji tu, bali pia yatakufanya kujisikia nafuu haraka zaidi kuliko dawa nyingine nyingi za kutibu aleji za viwandani zilizopo sokoni. 

  1. Ni mafuta mazuri kwa ngozi

Iwe ni mwonekano au afya ya ngozi kwa ujumla, ipo sababu kwanini watu wanapenda kuwa na ngozi ya kupendeza na yenye afya. Mafuta ya habbat soda yana asidi mafuta muhimu zaidi, yana vitamini nyingi, viondoa sumu vya kutosha na asidi amino muhimu ambazo miili yetu huzihitaji. Mafuta haya ni safi kwa ngozi kwa nyakati zote za siku na kwa siku zote. Pia yanasaidia ngozi kutokuungua moja kwa moja na miale ya jua huku yakizuia usizeeke haraka kwa kuondoa mikunjo yoyote kwenye ngozi yako. 

  1. Hutibu saratani ya ngozi (Melanoma)

Saratani ni matokeo ya kinasaba cha damu (DNA) kujizidisha au kujizalisha mara nyingi na kwa haraka zaidi dhidi ya uwezo wa kinga ya mwili. Mafuta ya habbat soda yana virutubishi vingine viwili ambavyo ni ‘thymoquinone’ na ‘thymohydroquinone’ ambavyo utafiti unaonyesha huwa vina uwezo wa kudhibiti saratani mbalimbali mwilini. Hii ni kutokana na sifa yake katika kuzuia uvimbe na bakteria, sifa kuu mbili za habbat soda.

Hufanya hivyo kwa kuzilenga seli nyeupe za damu kwa kuziongezea kinga ya mwili na hivyo kuua seli za saratani. 

  1. Hutibu chunusi

Chunusi ni matokeo ya moja kwa moja ya vivimbe kwenye ngozi hasa ya paji la uso na usoni kwa ujumla. Mafuta haya yanaondoa uvimbe wa aina yoyote kwenye ngozi na kuitengeneza upya ngozi huku yakiiacha nyororo na muonekano wake wa asili. Mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika kwa ajili ya kutunza na kutibu maradhi mbalimbali ya ngozi.

Usikose kuona magonjwa mengine wiki ijayo.

Angalizo: usiyatumie bila kuwasiana na tatibu wa dawa asili.

Makala hii imeandaliwa na Fadhili Paulo ambaye ni tabibu wa tiba asili. Kwa mawasiliano tuma ujumbe wa WhatsApp kupitia +255769142586.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles