Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
PRODYUZA wa muziki wa kimataifa Harmony Samuels a.k.a H Money, ameachia wimbo wake mpya uitwao “Tic Tik” akiwa amemshirikisha gwiji kutoka Nigeria, Reekado Banks.
Katika wimbo huo wenye mikito ya Kinigeria, ladha tamu kutoka kwa H-Money akiungana na Reekado, unatengeneza burudani ya aina yake ya mtindo wa Afrobeats uliotayarishwa kwa umaridadi wa hali ya juu.
“Tic Tik” inaashiria mwanzo mpya wa muziki kwa H-Money ambaye amewahi kufanya kazi na wasanii kama Ariana Grande, Jennifer Lopez, Maroon 5, Rick Ross, Fifth Harmony, Mary J. Blige na wengine wengi.
Akizungumzia wimbo huo, H-Money anasema: “Tic Tik ni wimbo wangu wa kwanza katika mwanzo mpya wa muziki mzuri wa AfroBeats ukiwa kwenye mchanganyiko wa R&B, unaozingatia tamaduni zetu huku nikiwashirikisha wasanii wakali kwenye muziki.”
Wimbo huo siyo tu kwamba unaonyesha ushirikiano wa kusisimua kati ya wasanii wawili wenye nguvu kubwa katika muziki, lakini pia unatumika kama hatua muhimu katika safari ya kisanii ya H-Money anapojitosa katika ulimwengu mahiri wa Afrobeats.