28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Griffin awaomba radhi mashabiki

Griffin2015NEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa mpira wa kikapu wa timu ya Los Angeles Clippers, Blake Griffin, amewaomba radhi mashabiki kwa kitendo cha kushiriki tukio la ugomvi.

Ugomvi huo ulimpelekea mchezaji huyo kuvunjika mkono wa kulia na hivyo atakaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki nne hadi sita kuuguza mkono huo.

Hata hivyo, uongozi wa Ligi ya NBA unaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo ambalo lilitokea siku ya Jumamosi mwishoni mwa wiki iliyopita, nje ya mgahawa wa Toronto, nchini Marekani.

Griffin, ambaye ni nyota mara tano wa timu ya All Star, alionekana kujitokeza katika vurugu hizo na alivunjika wakati anajilinda aliporushiwa mzingo ambao ulikuwa na vitu vizito ndani yake na kusababisha kuvunjika.

“Naanza kwa kuomba radhi kwa taasisi ya Clippers, wachezaji wenzangu na mashabiki wote wa kikapu, nilishiriki katika jambo ambalo sikulitarajia kama ningepata madhara kama haya ya kusababisha kukaa nje ya uwanja kwa muda, lakini ninaamini nitaendelea vizuri na nitarudi uwanjani muda mfupi ujao,” alisema Griffin.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles