27.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

Man City kupambana na Liverpool fainali

02man-cityMANCHESTER, ENGLAND

KLABU ya Manchester City imefanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya ushindi wa juzi dhidi ya Everton wa mabao 3-1 katika michuano ya Kombe la Capital One hatua ya nusu fainali, huku fainali watakutana na Liverpool, Februari 28, kwenye Uwanja wa Wembley.

Klabu hiyo imekuwa ya pili kuingia hatua hiyo baada ya Liverpool kuwa ya kwanza kufanikiwa kuingia kwa kuichapa Stoke City mabao 6-5 kwa mikwaju ya penalti.

Katika mchezo wa Manchester City, klabu ya Everton ndio walikuwa wa kwanza kucheka na nyavu za wapinzani wao baada ya kiungo wao, Ross Barkley kuifungia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 18 ya mchezo huo.

Kiungo kutoka Brazil, Fernandinho, alifanikiwa kusawazisha bao hilo kwa shuti kali baada ya kupata nafasi katika dakika ya 25.

Hata hivyo, kiungo mshambuliaji wa Man City, Kevin De Bruyne, alifanikiwa kuongeza bao la pili baada ya kuunganisha mpira ambao ulipigwa na Raheem Sterling, wakati huo mshambuliaji wao hatari, Sergio Aguero, aliongeza bao la tatu na kunyamazisha kelele za wapinzani wao.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika kwenye Uwanja wa Goodson Park, Everton wakiwa nyumbani walifanikiwa kushinda mabao 2-1.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles