22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, October 6, 2022

Giroud kuikosa Liverpool

KIKOSI cha AC Milan kitasafiri bila Olivier Giroud, kitakapokwenda England kuivaa Liverpool katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya mchezaji huyo kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Timu hizo zitavaana Septemba 15, mwaka huu, na ni pigo kwa eneo la ushambuliaji la Milan kwa kuwa Zlatan Ibrahimovic naye anauguza majeraha ya goti.

Nyota huyo wa zamani wa Chelsea ameanza vizuri maisha yake ndani ya kikosi cha Milan kwani ameshafunga mabao mawili katika mechi mbili za msimu huu wa Serie A.

Kabla ya mechi hiyo dhidi ya Liverpool, Giroud atakuwa karantini wakati Milan ikimenyana na Lazio (Septemba 12).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,814FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles