22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Gigy Money atembelea banda la WinPrincess

Na Jeremia Ernest, Mtanzania Digital

DIVA wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Gift Stanford maarufu ‘Gigy Money‘ ambaye ni Balozi wa kampuni ya kubashiri ya WinPincess ametembelea banda lao katika viwanja vya sabasaba akiwa na washiriki wa Miss Tanzania 2023.

Akizungumza na wandishi wa habari Julai 9, katika banda la WinPreses, ameeleza faida za kucheza mchezo huo kupitia simu ya mkononi bila ya kwenda katika kumbi za kubashiri.

“Ukibashiri kupitia WinPrincess, hakuhitaji garama kubwa ni kuanzia Sh 10,000 na hakuna nauli kwa kuwa unacheza kupita simu yako ya kiganjani na pesa unapata papohapo bila longolongo, hitaji kubwa ni kuwa na akaunti ya WinPrincess,” amesema Gigy Money.

Aidha, Gigy Money, aliushukuru uongozi wa WinPrincess, kwa kuchagua kudhamini shindano la Miss Tanzania, katika upande wa michezo kwa sababu jukwaa hilo limekuwa likiinua vipaji vya watoto wa kike.

“Najivunia kuwa familia ya WinPreses, kwa sababu wanapenda maendeleo ya jamii yangu leo hii wameingia kufahamu shindano kubwa la Miss Tanzania ambalo limetoa mastaa wengi na bado linaendekea kuzalisha vipaji vipya,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles