26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

GGML yaibuka kampuni kinara inayozingatia malengo ya SDGs

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya AngloGold Ashanti – Geita Gold Mining Limited (GGML) imeibuka mshindi wa jumla katika tuzo za kampuni za kibiashara zilizoonesha kwa vitendo mchango wake kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwenye kipengele cha kujali watu.

Mkurugenzi wa Bodi ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Felix Mlaki (kulia), Makamu Rais wa AngloGold Ashanti anayesimamia miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo (kushoto), Meneja Mawasiliano wa GGML, Stephen Mhando (wa pili kulia) na Ofisa Utawala, Layla Mohamed wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuibuka mshindi wa jumla katika kipengele cha kampuni ya kibiashara inayohali watu. Tuzo hizo za SDGs zimetolewa na Shirika la UN Global Compact Tanzania.

Tuzo hiyo iliyotolewa na Shirika la UN Global Compact Network Tanzania Aprili 29, 2023 jijini Dar es Salaam, imetajwa kuthibitisha nia ya GGML kujitolea kuzisaidia jamii zinazozunguka mgodi huo, pamoja na kuimarisha mazingira mahali pa kazi kuwa salama na shirikishi huku wafanyakazi wake wakitekeleza majukumu yao kwa kuzingatia utu.

Akipokea tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Bodi ya GGML, Felix Mlaki alisema: “Tuzo hii ni ushuhuda wa dhamira yetu ya kusaidia jamii inayozunguka mgodi wetu, pamoja na juhudi zetu za kuwa na mahali pa kazi panapozingatia afya na usalama kwa wafanyakazi wetu.

Aliendelea kusema kuwa baada ya kupata tuzo, kampuni hiyo itaendelea kuimarisha dhamira yake kama sehemu ya Uwajibika wa kampuni kwa Kijamii (CSR) kwa kutekeleza miradi inayofanana na juhudi za serikali katika kuendeleza jamii. 

“Tuzo hii inatambua juhudi zetu za kuheshimu haki za binadamu na uendelevu wa mazingira huku tukishirikiana na jamii kutekeleza miradi mbalimbali kupitia mpango wa uwajibikaji wa jamii kwa jamii,” amesema.

Alibainisha kuwa kampuni itaendelea kuboresha maisha ya wakandarasi wa ndani, ikiwa ni pamoja na kuwapa kipaumbele katika fursa za zabuni ili waweze kuchangia upatikanaji wa ajira kwa watanzania wengi katika shughuli za uchimbaji madini.

Tuzo hizo zilizozinduliwa Februari mwaka huu zinalenga kuendeleza ushirikiano kati ya wadau wa sekta binafsi na Serikali katika utekelezaji malengo ya maendeleo endelevu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles