25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

TTB yawataka watoa huduma sekta ya utalii kutoa huduma bora

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Damas Mfugale amewataka watoa huduma sekta ya utalii watoe huduma bora ili ziwavutie watalii waweze kurudi nchini.

Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina ya waandishishi wa habari kuhusu utalii Mkurugenzi Mfugale alisema Kutokana na taalumu yao watumia kuhamasisha utalii nchini kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Damas Mfugale.

“Kutangaza utalii pekee yake haitoshi tunahitaji kuboresha huduma na ubora wa huduma ni jambo lingine huduma nzuri zitawafanya watalii kuwa mabalozi wazuri,” alisema Mfugale.

Alisema waandishi wa habari ni watu muhimu katika kukuza sekta hiyo na wanafasi kubwa ya kutangaza mitandaoni ndani na nje ya nchi

“Utalii ni biashara ambayo ikifanyika kwa waledi itasadia kukuza uchumi kwa sasa pato la taifa utalii unachangia kwa asilimia 17,” alisema Mfugale.

Mfugale alisema ikiwa leo umetimia mwaka mmoja wa “Royal tour ” watilii ni wengi wanaokuja nchini.

Naye Rais Chama cha Waandishishi Mtandaoni, Simon Mkina alisema lengo la semina hiyo ni kuongeza mapato kupitia mitandao ya kijamii.

“Waandishi wa habari wa mitandaoni kutumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kutangaza utalii kwa kuandika habari za utalii na kuvutia watalii,” alisema Mkina.

Naye Mkufunzi Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), Amri Abdi alisema mafunzo hayo yatasaidia kukuza uchumi kupitia utalii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles