28.4 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

GF Trucks yaipiga tafu Geita Gold Fc

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Kampuni ya uuzaji wa magari makubwa na mitambo ya GF Trucks imeingia udhamini wa mwaka mmoja wa kuidhamini timu ya soka ya Geita Gold Fc.

Udhamini huo ambao umesainiwa Dar es Salaam Septemba mosi, mwaka huu mbele ya Katibu Mkuu wa Geita Gold, Simon Shija.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika makubaliano hayo Afisa Biashara Mkuu wa GF Truck, Salman Karmali amesema wamefikia hatua hiyo baada ya Geita Gold kufanya vyema kwenye ligi kuu ya NBC.

Pia ameeleza mbali na kufanya vyema kwa sasa timu hiyo inawakilisha nchi katika mashindano ya Kimataifa hivyo wameiongezea nguvu ili kupeperusha vyema bendera ya Taifa la Tanzania.

“Geita Gold inawakilisha nchi yetu, hivyo tumeona tuwaongezee nguvu ili kuitangaza nchi yetu,” amesema Karmal.

Naye Katibu Mkuu wa Geita Gold, Simon Shija amesema wanaishukuru GF Trucks kwa kuwaongezea nguvu huku wakihimiza kampuni nyingine kusaidia timu hiyo.

Geita Gold Fc iliyopo chini ya Halmashauri ya Geita inatarajiwa kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles