25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

GESI MIHAN LPG YATHAMINI MAISHA YA MTANZANIA

Muuzaji wa rejareja wa Mihani Gesi
Muuzaji wa rejareja wa Mihani Gesi

Na Mwandishi Wetu,

Misitu ni muhimu kwa maisha ya binadamu na viumbe hai kwakua huifadhi vyanzo vya maji, kuboresha hali ya hewa, kuzuia mmomonyoko wa ardhi, upatikanaji wa mbao, madawa na malisho ya mifugo.

Misitu huboresha shughuli za kilimo na kuboresha mandhari ya nchi yetu mijini na vijijini, aidha pia ni chanzo muhimu cha mapato kwa wananchi wengi wa vijijini na mijini.

Iko wazi kuwa kuna utegemezi mkubwa wa misitu kama chanzo kingi, rahisi na kikuu cha nishati nchini, ambapo zaidi ya asilimia 90 ya nishati inayotumika nchini inatokana na miti.Lakini kwa gharama kubwa ya mazingira.

Uvunaji mkubwa wa mkaa umeathiri sana ubora wa misitu, kuni zinatumika zaidi vijijini na mkaa unatumika zaidi mijini.

Matumizi ya nishati ya gesi ni suluhisho la tatizo hilo, katika kukabiliana na tatizo la uharibifuwa misitu,  Mihan Gas na wadau wa sekta mbalimbali hasa  Wizara ya Nishati na Madini na jamii kwa ujumla wanashirikiana ili kupunguza utegemezi wa misitu kama chanzo kikuu cha nishati ya kupikia majumbani.

Zifuatazo ni faida za kutumia gesi ya ‘Mihan Gas’.

Usalama

Mitungi ya Mihan gas inayo valvu salama (safety valve) ili kuzuia isilipuke ikiwa msukumo wa gesi ndani ya mtungi imepanda; kwani valvu salama inafunguka na kufunga kwa sekunde chache ilikupunguza msukumo mpaka kiwango salama na hivyo gesi hii inazuia mitungi isilipuke.

Kampuni ya Mihan gesi imekuja na suluhisho kwa ajili ya usalama wako na familia yako kwa kukuletea ‘mitungi yenye valvu salama’.

Unafuu wa gharama

Matumizi ya gesi ni nafuu ukilinganisha gharama za mkaa ambao unapatikana kwa gharama kubwa kwa ujumla wake, matumizi ya gesi kwenye upishi ni bora na haraka kuliko mkaa, unaokoa gharama na unapata uhakika wa mapishi yako nyumbani muda wote.

Gesi ya Mihan inauwezo wa kuchoma mara nne zaidi ya nishati ya mkaa na kuni hivyo kuifanya nishati hii kuwa bora zaidi katika kuokoa gharama za juu katika matumizi ya kilasiku.

Mazingira na usafi

Gesi ya Mihan  haichafui mazingira, ni rafiki kwa mazingira kwa kuwa haitoi hewa chafu na haiharibu mazingira ukifananisha na nishati nyingine kama mkaa, kuni na kadhalika.

Gesi haisababishi uchafu kwenye nyumba yako pia na vyombo vyako vya kupikia (sufuria) kwa kuwa haisababishi moshi wala masizi hiyo kuifanya nishati hii kuwa bora, safi na rafiki kwa matumizi ya nyumbani kwako kwa kuwa haisababishi uchakavu wa vyombo na vifaa vyako kwa ujumla.

Afya

Matumizi ya gesi ya Mihan ni rafiki kwa afya ya binadamu kwa kuwa haina moshi wala harufu mbaya hivyo nishati hii ni bora kwa matumizi yako ya nyumbani ukilinganisha na mkaa na kuni ambayo harufu hubaki mwilini na pia pamoja na hayo magonjwa ya mapafu huepukika kwa kuwa hakuna moshi utakaotoka kwenye jiko lako la gesi hivyo basi kuifanya nishati kuwa bora zaidi

Inaokoa muda na rafiki kwa matumizi

Mihan Gas huokoa muda kwa mtumiaji kutokana na miundombinu ya nishati hii na uwezo wake wakutumika na haina haja ya matayarisho kama nishati ya mkaa.

Matumizi ya jiko la gesi ni rafiki kwa kuwa liko tayari muda wowote kutumika linapohitajika bila kujali muda, hali ya hewa na vikwazo vingine; mapishi yake ni ya haraka na huivisha vyema na kupata harufu nzuri na ladha bora ya chakula kwa kuwa gesi huchoma haraka na kuivisha vizuri wakati wa mapishi hivyo ni rafiki kwa mapishi ya nyumbani na biashara.

Gesi ya Mihan haipotei

Mihan Gas hudumu kwa muda mrefu kwa kuwa ni nishati ambayo imetengenezwa na miundombinu inayowezesha kuitunza vyema na haipotei wakati na baada ya matumizi.

Ni Mihan Gas inayothamini maisha ya kila Mtanzania ndio maana inajaribu kuelemisha umuhimu wa kutumia gesi ambayo moja kwa moja inamlenga kila mwananchi nchini kote kwenye mtandao uliojitosheleza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles