24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Geita Gold FC. matumaini kibao wakiwavaa Wasudan

Na Mwanadishi Wetu, Mtanzania Digital

MATAJIRI wa madini, Klabu ya Geita Gold kesho wanatarajia kurusha karata yao ya kwanza katika michuano ya kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa kuwavaa Hilal Alsahil ya nchini Sudan Kaskazini.

Geita Gold FC ambao watakuwa ugenini katika mechi hiyo ya raundi ya mchujo wa kwanza mzunguko wa kwanza itapigwa Jumapili Septemba 11, mwaka huu saa mbili usiku katika uwanja wa Al-Hilal, jijini Khartoum.

Kwa mujibu wa Afisa Habari mwandamizi wa timu hiyo, Hemed Kivuyo matajiri hao wa dhahabu kutoka Geita, tayari wameondoka nchini alfajiri Septemba 9, 2022 kwa ndege kupitia Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuelekea nchini Sudan.

Kivuyo amesema timu hiyo imeondoka na msafara wa wachezaji 22, viongozi watano wakiwamo benchi la ufundi, Kocha Mkuu, Freddy Felix Kataraiya Minziro na kocha msaidizi Julius Wandiba.

“Timu imeondoka kwa morali kubwa na mwalimu ametuahidi kwamba atahakikisha anacheza mchezo wa kujihami zaidi ili wasifungwe na wakirejea nchini tumalize mchezo.

“Tunawashukuru TFF wametusaidiaa kukamilisha taratibu zote za COVID, lakini pia tunawashukuru kwa dhati kabisa wafadhili GGML kwa kugharamia kambi ya timu pamoja na kulipia tiketi za  kwenda na kurudi sambamba na gharama nyingine safari nzima ya timu kuelekea na kurejea Sudan,” amesema.

Geita Gold FC ambao wamefadhiliwa na Kampuni ya Uchimbaji Madini Geita (GGML) wamepiga kambi jijini Dar es Salaam na  wanatarajiwa kurudiana na Wasudan hao siku nne baada ya mechi hiyo ya kwanza.

Mshindi wa mchezo huo kati ya Geita Gold na Hilal Alsahil atakutana na Pyramids FC ya nchini Misri kwenye hatua inayofuata.

Geita Gold ambao walipanda daraja msimu wa 2020/2021, wawanashiriki kwa mara ya kwanza michuano ya kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles