28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

Rais Samia atunukiwa Tuzo Nigeria

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digiatal

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amepokea tuzo ya heshima ya Pyne Africa Awards 2022 katika hafla iliyofanyika kwenye viunga vya Eko Hotels na Suites, jijini Lagos, Nigeria.

Rais Samia ametunukiwa tuzo hiyo baada ya kuchaguliwa kama Rais bora muwajibikaji katika kuiendeleza sekta ya utalii barani Africa.

Tuzo hii imepokelewa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini Nigeria, Dk. Benson Alfred Bana kwa niaba ya Rais. Halfa hii ilihudhuriwa pia na Meya Mkuu wa Zanzibar, Mahomoud Mussa na Mwenyekiti wa Tume ya Utalii Zanzibar, Rahim Bhaloo.

Aidha, Rais, wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea tuzo ya heshima kwa kutambua mchango wake wa mfano katika kukuza sekta ya Utalii Zanzibar ambayo ni kivutio cha Utalii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,691FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles