25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Wananchi Misenyi wahimizwa kutunza miundombinu ya maji

Na Renatha Kipaka, Misenyi

Wananchi wilayani Misenyi mkoani Kagera wametakiwa kutunza miundombinu ya maji, huku wakiamini kwamba Serikali imetumia ghrama ya kufanikisha upatikanaji wa huduma hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nadhifa Kemikimba wakati akiwa kwenye mradi wa maji wilayani Misenyi utakaonufaisha vijiji vya Rutunga na Rwamachu kata Buyango.

“Serikali inawekeza kwa kuwapatia miundombinu wananchi wake kwa kuweka bomba la kusukuma maji hizo ni fedha, hivyo wananchi wajue pia kuna gharama za uchangiaji,” amesema Kemikimba.

Amesema zipo gharama ambazo zinafanywa na serikali lakini zile za uendeshaji ni za wananchi wenyewe kwenye maeneo yao.

“Sisi tunasaidia tu kwenye uwekezaji na huduma kuwa endelevu, lakini zile za uendeshaji zinachangiwa na wao mambo ya ufundi ni serikali,” amesema Kemikimba.

Amefafanua kuwa bado kuna vijiji 12,380 nchini ambavyo vinatakiwa wananchi wapate maji safi na salama kwani yanatoka katika ardhi ya kutengenezwa miundombinu salama.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maji kata Buyango, Elias Kamala amesema kuwepo na miradi hiyo itasaidia wananchi kuacha kuzunguka milima kutafuta maji na kuithamini miundombinu inayosongezwa karibu yao.

“Wengine wanakwenda zaidi ya km moja kufuata maji, hivyo kupitia miradi inayowekwa na serikali tutafanya wananchi hata wavute maji majumbani,”amesema Kamala.

Kwa upande wake Mtendaji wa Kata Buyango, Pius Munyoya amesema katika suala la usalama wa miundombinu hiyo upo ushirikiano na Wakandarasi wanaotekeleza shughuli hiyo unafanyika kikamilifu.

Meneja wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijiji (RUWASA) wilaya ya Misenyi, Mhandisi Andrew Kilembe amesema mradi unatekelezwa kwa vyanzo vya pesa ya Uviko-19 na mpango wa lipa kwa matokeo(P4R)kwa garama ya zaidi ya Sh milioni 500.

Amesema ujenzi wa tanki katika kituo cha kuchotea maji unaendelea kwa kulaza mabomba na kufunga sola kwenye njia ya mitambo nakwamba unatarajiwa kukamilika Septemba 20 , mwaka huu na utanufaisha wananchi 3,912.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles