29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

GAZETI LA MAWIO LASHINDA KESI MAHAKAMANI

Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam


GAZETI la Mawio linatarajiwa kurejea mtaani Alhamisi ya wiki hii baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuyatupa maombi ya Serikali ya kulifuta gazeti hilo na kwamba hatua hiyo haikuwa sahihi.

Uamuzi huo ulitolewa hivi karibuni na jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Sakieti Kihiyo, Jaji Ignas Kitusi na Jaji Ama-Isario Munisi.

Akisoma uamuzi huo Jaji Kitusi alisema mahakama imeyatupa maombi ya Serikali kwa sababu Gazeti la Mawio halikupewa nafasi ya kujitetea kabla ya hatua ya Serikali ya kulifuta kutoka orodha ya msajili wa magazeti nchini.

Serikali ililifuta gazeti la MAWIO Januari 15, mwaka jana baada ya kudaiwa kuandika ilichoita habari na makala za “kichochezi”.

Utawala wa Kampuni ya Victoria Media Services Limited, wachapishaji wa gazeti la MAWIO, uliamua kufungua kesi namba 15 ya mwaka 2016.

Mkurugenzi Mtendaji na Mhariri Mkuu wa gazeti hilo, Simon Mkina alisema alishangazwa na hatua ya Serikali kufuta alichoita “mdomo wa wananchi”.

Mkina alisema MAWIO limekuwa gazeti linalozingatia maadili na kufuata weledi wa hali ya juu katika kuandika na kuchapisha habari na makala.

 Asema kufuatia uamuzi huo wa Mahakama, MAWIO litarejea mtaani Alhamisi ya wiki hii na kuahidi kuwapa wasomaji wake habari zilizofanyiwa kazi ya ziada kila Alhamisi.

“Kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja, gazeti wakati halipo mtaani – likiwa limefutwa na Serikali, pamoja na kupoteza ajira za watu na kuingia katika hasara kubwa, bado tulikuwa na kazi ya kujiuliza ni wapi tulikosea na je, lini tutapewa haki yetu? Bahati nzuri haki yetu imefika,” alisema Mkina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles