Kulwa Mzee, Dar es Salaam
Vigogo wa IPTL, Harbinder Sethi na James Rugemarila, wamekwama kufikishwa mahakamani leo asubuhi kwa sababu ya shida ya usafiri.
Hayo yamebainika leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati kesi hiyo ilipokuwa inatajwa bila washtakiwa kuwepo.
Wakili wa Serikali Emmanuel Nitume, alidai mahakamani kwamba washtakiwa hawapo mahakamani kwa sababu ya shida ya usafiri hivyo aliomba kesi iahirishwe.
Baada kuwasilisha hoja hiyo mahakama iliahirisha kesi hadi Desemba 6, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
Washtakiwa katika kesi hiyo wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi ikiwamo ya utakatishaji fedha.