26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Gari lakwamisha vigogo IPTL kufikishwa mahakamani

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Vigogo wa IPTL, Harbinder Sethi  na James  Rugemarila, wamekwama kufikishwa mahakamani leo asubuhi kwa sababu ya shida ya usafiri.

Hayo yamebainika leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati kesi hiyo ilipokuwa inatajwa bila washtakiwa kuwepo.

Wakili wa Serikali Emmanuel Nitume, alidai mahakamani kwamba washtakiwa hawapo mahakamani kwa sababu ya shida ya usafiri hivyo aliomba kesi iahirishwe.

Baada kuwasilisha hoja hiyo mahakama iliahirisha kesi hadi Desemba 6, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa katika kesi hiyo wanakabiliwa na  mashtaka 12 ya uhujumu uchumi ikiwamo ya utakatishaji fedha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles