Pawasa kufuta machozi Watanzania soka la ufukweni

0
1156

Winfrida Mtoi, Dar es Salaam

Kocha mkuu wa timu ya beach soka ya Tanzania, Boniface Pawasa ameahidi kufuta machozi ya Watanzania yaliyotokana na matokeo mabaya ya timu za taifa za mpira wa miguu Taifa Stars na Kilimanjaro Warrious U-23.

Pawasa amesema timu yake ya soka la ufukweni, itacheza na timu ya Uganda, Malawi na Shelisheli katika michuano ya Copa Dar es Salaam michezo itakayoanza kesho Novemba 22 kwenye fukwe za Coco beach.

“Watanzania wameudhunika mno na mashindano yetu yanayoanza kesho nawaahidi nitawafuta machozi na machungu yote wasijali waje kwa wingi kwenye mashindano yetu watuunge mkono kwenye fukwe za Coco beach,” amesema Pawasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here