27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Gareth Bale apata mtoto wa kike

Gareth-BaleMADRID, HISPANIA

NYOTA wa klabu ya Real Madrid na timu ya Taifa ya Wales, Gareth Bale, amefanikiwa kupata mtoto wa kike na kumpa jina la Nava Valentina.

Mchezaji huyo ameshindwa kujiunga na timu ya Taifa ambayo inatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Kaskazini Ireland na Ukraine kutokana na kuiangalia familia yake.

Hata hivyo, Bale mwenye umri wa miaka 26 alikuwa majeruhi kwa muda mrefu lakini kwa sasa ameanza kukitumikia kikosi cha Real Madrid.

Kupitia akaunti ya Instagram na Twitter, mchezaji huyo ameiweka picha yake akiwa na mtoto huyo na kummwagia sifa.

“Asante kwa kupata mtoto wangu wa pili, wewe ni mrembo umekuja kwa ajili ya kuiongezea familia yetu ukubwa, nakupenda sana Nava Valentina Bale,” aliandika Bale.

Huyo atakuwa ni mtoto wa pili kwa mchezaji huyo na mke wake Emma Rhys-Jones, huku wa kwanza akiwa na umri wa miaka mitatu ambaye anajulikana kwa jina la Alba Viola, alizaliwa Oktoba 2012.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles