26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Fifa kumchunguza Beckenbauer

Franz BeckenbauerZURICH, USWISI

SHIRIKISHO la Soka Duniani (Fifa), linamchunguza aliyekuwa nahodha na kocha wa timu ya Taifa ya Ujerumani, Franz Beckenbauer, kuwa miongoni mwa watuhumiwa waliohusika kutoa hongo ili kuwa wenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2006 nchini humo.

Kamati ya maadili ya Fifa imetoa orodha wa watu sita walioongoza kampeni hiyo ya kutwaa uenyeji wa Kombe la Dunia.

Hata hivyo, kiongozi huyo baada ya kubanwa na shirikisho hilo alikiri kufanya makosa wakati wa kuwania nafasi hiyo, ambapo Ujerumani ilifanikiwa kuwa wenyeji kwa kuwashinda Afrika Kusini kwa kura moja, ikiwa 12 kwa 11 katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2000.

Watuhumiwa wengine ambao wametajwa kuwa katika orodha hiyo ni pamoja na Wolfgang Niersbach wa nchini Ujerumani, Helmut Sandrock, Theo Zwanziger ambaye ni mwanasheria nchini humo, Horst Schmidt na Stefan Hans.

Hata hivyo, jarida moja nchini humo, Der Spiegel, mwaka jana liliripoti kuwa waandaaji wa kombe hilo walitenga Euro milioni 6.7 kwa ajili ya kununua uenyeji wa mashindano hayo.

Kwa upande wao, Niersbach na Sandrock, wanachunguzwa kwa kosa la kushindwa kuripoti ukiukwaji wa kanuni na maadili ya Fifa.

Beckenbauer alikiongoza kikosi cha taifa cha Ujerumani Magharibi wakati huo wakitwaa Kombe la Dunia la mwaka wa 1974.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles