27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Gadiel amwaga siri balaa linalofanywa na Simba

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

BEKI wa Simba Gadiel Michael, amesema tayari wachezaji wamesha kaa kikao kuweka mikakati ya kuendeleza kasi yao ya ushindi katika michezo yao ikiwamo ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho Afrika.

Gadiel ametoa kauli hiyo leo Novemba 30,2021 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wao dhidi ya Geita Gold, utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Wekundu wa msimbazi hao wataifaa Geita wakiwa wametoka kupata ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Red Arrows ya Zambia katika mchezo wa Kombe Shirikisho Afrika kwenye uwanja huo.

Beki huyo amesema wanataka kuendeleza moto wao ule ule wa tangu walipopata ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Ku una Ruvu Shooting, CCM Kirumba, Mwanza.

“Kasi yetu ni ile ile hakuna kupoa, wachezaji tumeshakaa vikao vyetu tumezungumza, naamini hakuna kitachoharibika tunahitaji ushindi,” amesema Gadiel.

Kuhusu kukosa nafasi kikosi cha kwanza, Gadiel amesema  ipo siku atapata nafasi na kuonesha uwezo wake kwa sababu anafanya mazoezi ya vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles