25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

G. Nako kuachia ‘Original’ leo

G. NakoNA THERESIA GASPER

MSANII wa muziki wa hip hop nchini kutoka kundi la Weusi, George Mdeme ‘G. Nako’, amesema video yake mpya inayojulikana kwa jina la ‘Original’ anatarajia kuiachia leo.

Msanii huyo amedai kwamba video hiyo inalenga watu ambao wanaishi maisha ambayo sio halisi.

Akizungumza na MTANZANIA jana,  G. Nako alisema kupitia video hiyo amewapa somo watu kuishi maisha yao halisi tofauti na yale ya kuigiza.

“Nina imani mashabiki wangu wataipokea vizuri video hii kwani ipo kimataifa na itawasaidia wengi kutokana na somo nililolitoa ndani ya video hiyo kama vile watu kuishi katika maisha yao halisi na sio ya kuigiza kama baadhi ya watu wanavyofanya,” alisema G. Nako.

Nako amedai kwamba video hiyo ameifanyia nchini Afrika Kusini chini ya mtayarishaji, Justin Campos huku audio akiwa ameifanyia hapa nchini mtayarishaji akiwa Nahreel.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles