25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

FOMU YA URAIS DRC YAUZWA MILIONI 200/-

 

KINSHASA, DRC


PAMOJA na fomu ya kuwania urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuuzwa bei ya juu ya Dola za Marekani 100,000 sawa na Sh milioni 224, wagombea 26 wamejitokeza kuwania wadhifa huo.

Hilo limefahamika siku moja baada ya Rais Joseph Kabila kutangaza kuachia ngazi, huku Tume Huru ya Uchaguzi DRC (CENI) ikitangaza orodha hiyo ndefu ya wagombea nchini humo.

Miongoni mwa wagombea hao ni wanawake watatu na mawaziri wakuu wa zamani watatu, wagombea huru wakiwa 16 na wa vyama vya upinzani wanane.

Daftari la kudumu la wagombea litatangazwa Septemba 19 tayari kwa maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika Desemba 23 mwaka huu.

Uchaguzi huo wa duru moja pekee umeorodhesha wagombea mara mbili zaidi kuliko ule wa mwaka 2011.

Juzi Jumatano pekee, ambayo ilikuwa siku ya mwisho kwa wagombea kuwasilisha majina yao, walijitokeza 18 pekee akiwamo mgombea aliyeteuliwa na Rais Kabila, Emmanuel Shadari.

Waziri huyo wa mambo ya ndani wa zamani amesema akichaguliwa atahakikisha wananchi wanaishi kwa amani na hali yao ya maisha kuboreka.

Naibu Katibu Mtendaji wa Chama tawala cha PPRD, Ferdinand Kambere, amesema uteuzi wa Shadary ni alama ya ushujaa wa demokrasia nchini.

Kwa upande wake upinzani umelezea kwamba uteuzi wa mgombea wa chama tawala, ni hatua ya ushindi wa demokrasia, lakini wametarajia mageuzi wakati wa uchaguzi.

Martin Fayulu ambaye ni mgombea wa vuguvugu Dynamique de l’opposition amesema raia ndie anayetakiwa kuamua kupitia uchaguzi huru.

Amesema hawana maoni yeyote kufuatia uteuzi huo wa mrithi wa Kabila, na kwamba ni mambo yao ya ndani, kwa kuwa Kabila anajua umuhimu wa maamuzi yake.

Amesema ikiwa amepanga njama ya kurejea madarakani baadae kama alivyofanya Rais wa Urusi Vladimir Putin na Waziri Mkuu Dmitry Medvedev hilo ni haki yake, lakini akionya kwamba wanachotaka uwepo wa uchaguzi huru, wa wazi na wa kidemokrasia ilikuruhusu raia wa Kongo kujichagulia viongozi wao wenyewe.

Miongoni mwa wagombea wa upinzani ni pamoja na Jeanpierre Bemba, Vital Kamerhe na Felix Tshisekedi kiongozi wa chama cha UDPS. Wagombea watatu ni wanawake ambao wawili wameishi ugenini akiwemo Bi. Monique Mukuna.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles