21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

GARI LA MBUNGE CHADEMA LAPATA AJALI, DEREVA AFARIKI

 

Na SEIF TAKAZA, SINGIDA


GARI la Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Magereli (Chadema) limepata ajali mkoani Singida, huku derava wa gari hilo akipoteza maisha kwa kufariki dunia.

Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia jana ambapo gari hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Yohana Kagina ambaye aligongana uso kwa uso na Fuso iliyokuwa ikitokea Singida kwenda Dar es Salaam.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike, alisema ajali ilitokea usiku wa kuamkia jana Agosti  9, saa 9.00 usiku katika eneo la Nkuhi Wilaya ya Ikungi mkoani hapa.

Alisema gari hiyo yenye namba za usajili T 348 CSR, ilikuwa ikitokea Dodoma kwenda Shinyanga ilipata ajali kwa kugongana na Fuso lenye namba za usajili T 237 CHE, ambapo dereva wake alifariki dunia papo hapo.

Kamanda Njewike, alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa fuso kuacha kuendesha upande wake na kuendesha upande wa kulia hivyo kusababisha  ajali  hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles