24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

FLOYD MAYWEATHER: UMRI UTANIPONZA

NEW YORK, MAREKANI

BINGWA wa ngumi uzito wa juu, Floyd Mayweather, amesisitiza kuwa umri wake unaweza kumpa wakati mgumu katika pambano lake dhidi ya Conor McGregor, Agosti 26, mwaka huu.

Mayweather amesema, anaamini pambano hilo litakuwa na ushindani wa aina yake lakini litakuwa tofauti na lile la miaka miwili iliyopita dhidi ya Manny Pacquiao.

Pambano hilo linatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa T-Mobile Arena, mjini Las Vegas, Marekani, lakini Mayweather amedai mpinzani wake, McGregor ana nafasi kubwa ya kuwa mshindi.

“Mpinzani wangu ana umri mdogo sana, ana miaka 29 na mimi nina miaka 40, ukiangalia kuna tofauti kubwa kati yetu, hivyo ninaelekea kuchoka na yeye bado ana nafasi ya kuendelea kuwa kwenye ushindani kwa kipindi kirefu.

“Naweza kusema kwamba mimi ni mzee sasa, nipo tofauti sana na miaka miwili iliyopita, hivyo chochote kinaweza kutokea kwenye pambano hilo, kila mmoja ana lengo la kushinda ili kuweka historia yake,” alisema Mayweather.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles