22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Fisi akamata mtoto mbele ya mama yake na kumuua

Abdallah Amiri -Igunga      

MTOTO Msali Jijanda mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu, mkazi wa Kijiji cha Isakamaliwa, Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, anadaiwa kuuawa baada ya kukamatwa na fisi wakati akicheza na wenzake mbele ya mama yao mzazi.

Akizungumza na MTANZANIA mjini hapa jana baba mzazi wa mtoto huyo, Jijanda Maguja, alisema tukio hilo limetokea juzi saa moja usiku.

Maguja alisema mtoto wake alikuwa akicheza na wenzake nyumbani kwake, lakini muda mfupi fisi alitokea na kumchukua, kisha kukimbia naye hadi vichakani.

Alisema baada ya kuondoka naye, mama yake Mboje Mwenda aliamua kumfukuza, lakini fisi alimwacha mtoto na kumrudia yeye na kujikuta akianguka na kuzimia, huku mbwa wakibweka kwa nguvu.

“Kitendo cha mama yake kuanguka, kilitoa mwanya kwa fisi kuondoka na mtoto jumla hadi walipofuatilia kesho yake,” alisema.

Maguja alisema siku ya pili, wananchi walifanya msako mkali bila mafanikio, lakini baadaye walifanikiwa kuona nusu ya mwili wa mtoto huyo kichakani, huku baadhi ya viungo kuanzia kiunoni kushuka chini vikiwa vimeliwa.

Alisema baada ya kuuona mwili wa mtoto huyo, wananchi walianza msako tena kwa kutumia pikipiki na kufanikiwa kumuona fisi huyo, lakini walimfukuza bila kumpata.

Diwani wa Kata ya Isakamaliwa, Dotto Kwilasa, alithibitisha kuuawa kwa mtoto huyo na kusisitiza kuwa wanaendelea kumsaka fisi huyo wakishirikiana na Idara ya Maliasili Igunga.

Ofisa Wanyamapori Wilaya ya Igunga, Imani Mwasongwe, alisema baada ya kupokea taarifa hiyo, walikwenda eneo la tukio kumsaka fisi bila mafanikio.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles