25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

Balozi wa Zimbabwe Tanzania matatani

Waandishi Wetu – DAR ES SALAAM

ZIMBABWE imeeleza kutofurahishwa na hatua ya Marekani kumuwekea vikwazo vya kusafiri Anselem Nhamo Sanyatwe, ambaye ni balozi wake nchini Tanzania.

Katika taarifa ya serikali ya Zimbabwe iliyotolewa jana imeitaja hatua hiyo ya Marekani kama inayorudisha uhuru wa taifa hilo.

Zaidi ilisema hatua hiyo inashinikiza migawanyiko badala ya kuleta uponyaji wa taifa na maelewano.

Wizara ya Mambo ya Nje Marekani ilitangaza vikwazo dhidi ya Balozi Sanyatwe, ambaye ni Brigedia mstaafu ya jeshi la kitaifa la ulinzi wa rais,  na mkewe kutokana na kuhusika kwake katika ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

Wizara hiyo Marekani imeeleza kuwa inazo taarifa za kuaminika kwamba Anselem Sanyatwe alihusika katika msako mkali dhidi ya raia Zimbabwe ambao hawakujihami wakati wa ghasia zilizozuka Agosti mosi mwaka jana baada ya Uchaguzi Mkuu, na kusababisha vifo vya watu raia sita.

Kutokana na hatua hiyo Zimbabwe imesema imepokea kwa uzito uamuzi huo wa baadhi ya mataifa yenye nguvu yaliojichukulia hatua binafsi.

Katika taarifa yake hiyo iliyotolewa jana Zimbabwe ilisema kuwa vikwazo hivyo ni kinyume cha sheria na kushinikizwa kwa hatua nyingine kama hiyo itakuwa haina manufaa.

Sanyatwe ambaye alikuwa mkuu wa kitengo cha jeshi la ulinzi wa rais, na sasa ni balozi wa Zimbabawe Tanzania aliushutumu upinzani kwa mauaji hayo katika ushahidi aliotoa mbele ya tume ya uchunguzi iliyongozwana rais mstaafu wa Afrika Kusini, Kgalema Motlanthe.

Agosti mosi mwaka jana ghasia zilizuka nchini Zimbabwe kati ya wafuasi wa upinzani na vikosi vya usalama katika mji wa Harare huku kukiwa na maandamano ya kupinga  kucheleweshwa kwa matokeo ya uchaguzi.

Magari yaliyobeba maji ya kuwatawanya waandamanaji na mabomu ya machozi yalitumiwa katika barabara muhimu za mji wa Harare baada ya wafuasi wa chama cha upinzani cha MDC Alliance kuweka vizuizi katikati ya mji huo.

Watu sita waliuawa katika maandamano hayo ya wafuasi wa chama cha upizani cha MDC mjini Harare.

Makundi ya waandamanaji yaliyokuwa katikati ya mji huo tangu alfajiri baada tu ya kutangazwa kwamba Zanu PF kimeshinda viti vingi katika bunge na kwamba matokeo ya urais hayakuwa tayari, hali ilibadilika.

Walifanya maandamano katika barabara muhimu mjini Harare na kuelekea katika ofisi za zamani za chama cha Zanu PF wakibeba mawe makubwa, fimbo.

Kundi hilo lilisema ‘tunamtaka Chamisa’, wakiamini kwamba uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu.

Matokeo yalionyesha kwamba Zanu-PF kilishinda viti vingi vya ubunge katika uchaguzi huo tangu kung’atuliwa madarakani kwa Robert Mugabe.

Chama cha upinzani cha muungano wa MDC kilisema udanganyifu umefanyika na kwamba mgombea wake Nelson Chamisa alikuwa ameibuka mshindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles