Filamu na tamthilia za Kichina zazinduliwa Dar

0
1181

BALOZI WA STAR TIMESNA MWALI IBRAHIM

KAMPUNI ya Star Times Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya vyombo vya habari, uchapishaji, redio, filamu na runinga ya Beijing wamezindua maonyesho ya filamu na tamthilia za kusisimua za Kichina barani Afrika.

Kaimu mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Yang Peili, akizindua maonyesho hayo jana katika ofisi za kampuni ya Star Times jijini Dar es Salaam, alisema Tanzania itabaki kuwa mshirika wake mkubwa na wataendelea kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili.

“Kwa makadirio, jumla ya filamu na tamthilia 30 za kwenye runinga zitaonyeshwa nchini Tanzania na nchi nyingine za Afrika, dhumuni kuu ni kuimarisha muunganiko wa mwingiliano wa kitamaduni baina ya marafiki zetu wa Afrika na watu wa China,” alisema Yang.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here