27.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Brendan Rodgers kibarua chake matatani

brendan rodgersLIVERPOOL, ENGLAND

BAADA ya Liverpool kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Norwich City, mashabiki wamemtaka bosi wa klabu hiyo kumfukuza
kocha wao Brendan Rodgers. Klabu hiyo mpaka sasa imefanikiwa kushinda michezo miwili kati ya sita iliyocheza
huku ikitoa sare miwili na kufungwa miwili.

Katika mchezo wa jana Liverpool ilikuwa nyumbani na kutoka sare dhidi ya klabu ambayo imepanda daraja msimu huu, hivyo mashabiki wa klabu hiyo wamemtumia ujumbe bosi wa klabu hiyo John Henry, kupitia akaunti yake ya Twitter.

Wengi wamesema wakati wa Rodgers kuifundisha klabu hiyo umekwisha na huu ni wakati wa kutafuta kocha mwingine wa kuweza kuchukua nafasi hiyo.

Hata hivyo, kutokana na malalamiko ya mashabiki, inasemekana kuwa tayari uongozi wa klabu hiyo umefanya mazungumzo na kocha wa klabu ya Dotmund ya nchini Ujerumani, Jurgen Klopp na kocha wa zamani wa
klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti.
kutokana na matokeo hayo mabaya, kocha huyo amewataka wachezaji wake kujituma zaidi ili kurudisha heshima ya klabu hiyo katika uwanja wa nyumbani.

“Ni kweli tumefanya vibaya katika michezo yetu, lakini ni wakati sasa wa kubadilisha matokeo katika michezo ijayo ili kuweza kurudisha heshima ya Uwanja wa Anfield.

“Anfield ni sehemu pekee ya sisi kuonesha uwezo wetu kisoka, tunatakiwa kuutumia vizuri uwanja wetu ili kuwapa
nguvu mashabiki ambao wanajitokeza uwanjani.

“Kwa upande wangu najisikia vibaya na matokeo ambayo tumeyapata, lakini ninaamini tuna kila sababu ya kubadilika na kufanya kile ambacho klabu inataka,” alisema Rodgers.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles