25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Filamu 80 kushindanishwa Tamasha la ZIFF mwaka huu  

pROFESA mHANDO ZIFFTHERESIA GASPER

JUMLA ya filamu 490 kutoka nchi 32 zimepokelewa kwa ajili ya Tamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF), linalotarajiwa kufanyika Julai 9 hadi 17 katika viwanja vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar.

Licha ya kupokelewa filamu hizo, filamu 80 tu ndizo zitakazoshindanishwa katika makundi matano maalumu ambapo 59 zitashindanishwa katika kundi la kawaida, 15 kundi la Sembene Ousmmane, 12 za Bongo movie na nyingine tano zipo kwenye kundi jipya la filamu zinazozungumzia Zanzibar ambapo tuzo yake itaitwa Emerson.

Filamu inayotarajiwa kufungua tamasha hilo ni ya Kalushi kutoka Afrika Kusini.

Mkurugenzi wa ZIFF, Profesa Martin Mhando, alisema jambo la kukumbukwa zaidi mwaka huu ni kuongezeka kwa jumla ya filamu za Tanzania katika mashindano hayo, ambapo filamu tano kati ya 17 zitashindanishwa kwa tuzo ya Ousmane Sembene.

Pia filamu kutoka Afrika Mashariki nazo zimeongezeka ambapo nane za Tanzania, tano za Kenya, tatu za Uganda na mbili za Rwanda na filamu tatu zitaonyeshwa kwa mara ya kwanza katika tamasha hilo.

Profesa Martin aliongeza kwamba katika tamasha la mwaka huu kutakuwepo na mashindano ya video za muziki ambazo zitatangazwa mwishoni mwa mwezi huu na hizo zitaonyeshwa katika maonyesho hayo,” alisema Mhando.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles