23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Bieber ashtakiwa kwa kuvunja simu

Justin Bieber In Concert At The MGM GrandTEXAS, MAREKANI

MWANAMUZIKI maarufu nchini Marekani, Justin Bieber, ameshtakiwa kwa kuvunja simu ya Robert Morgan na kutakiwa alipe dola 75,000.

Nyota huyo ametuhumiwa kuivunja simu hiyo aina ya iPhone kipindi Morgan anamrekodi Bieber wakati alipokuwa akinywa pombe katika bar ya Cle jijini Texas mwezi uliopita.

Kulingana na mtandao wa TMZ, inadaiwa kwamba msanii huyo alikasirishwa na kitendo cha kumrekodi wakati anakunywa pombe.

Hata hivyo, thamani ya iPhone hiyo haifiki dola 75,000, lakini anatakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha kwa sababu simu hiyo ilikuwa na picha ambazo haziwezi kupatikana tena ikiwemo picha za sherehe ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa bibi yake Morgan.

Morgan pia anadai kwamba alipoteza idadi kubwa ya namba zake za mawasiliano za wafanya biashara wenzake. Hata hivyo, Bieber bado hajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles