MKURUGENZI wa Kampuni ya Prime Time Promotion, Ruge Mutahaba, ameweka wazi kwamba Tamasha la Fiesta la mwaka huu litakalotimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake litakuwa na ubunifu mkubwa.
Ruge alisema kutokana na kutokufanyika kwa mwaka jana kulikotokana na kupisha zoezi la uchaguzi tamasha hilo kwa mwaka huu limeongezwa vionjo mbalimbali ili kuliweka tofauti na yaliyopita.
“Tumejipanga kutoa burudani za kutosha katika tamasha la mwaka huu kwa kuwa muda mrefu tumekaa kimya bila kufanya tamasha hilo hivyo tutarudi kwa kishindo tukiwa tumeliboresha vya kutosha ili kutoa burudani kwa wote,” alisema Ruge.