23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

FCS yaiomba Serikali kuangazia upatikanaji wa miundombinu ya kidigitali kwa makundi maalum

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Asasi za kiraia nchini, kupitia Shirika la The Foundation for Civil Society (FCS), zimeiomba Serikali kuhakikisha makundi maalum, hususan watu wenye ulemavu, wanapatiwa miundombinu ya kidigitali ili waweze kushiriki kikamilifu katika michakato ya maendeleo na kujijenga kiuchumi.

Ombi hilo lilitolewa na Meneja Programu wa FCS, Nasim Losai, katika mkutano wa kitaifa wa watu wenye ulemavu, madiwani, na wadau uliofanyika Agosti 12, 2024, jijini Dar es Salaam. Losai alisema kuwa mkutano huo ulilenga kuimarisha ushiriki wa watu wenye ulemavu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii, huku ukizingatia matumizi ya takwimu za sensa katika kuboresha mipango ya halmashauri na ngazi za kata.

Meneja Programu wa FCS, Nasim Losai akizungumza na waandishi wa Habari katika mkutano wa kitaifa wa watu wenye ulemavu, madiwani na wadau, uliofanyika Agosti 12, 2024 Jijini Dar es salaam.

Aliongeza kuwa, ingawa Serikali imekuwa sikivu katika kusaidia makundi maalum, bado kuna haja ya kuendelea kuboresha juhudi hizi, hasa kwa kuhakikisha upatikanaji wa fursa za kiuchumi kupitia miundombinu bora. FCS, kwa zaidi ya miaka 20, imekuwa ikisaidia serikali katika shughuli za kijamii na kutetea haki za watu wenye ulemavu.

Mshauri mtaalam wa masuala ya watu wenye ulemavu nchini, Peter Charles, alibainisha kuwa mkutano huo ulihudhuriwa na watu wenye ulemavu zaidi ya 600 pamoja na madiwani 60 wa viti maalum kutoka Jiji la Dar es Salaam. Mkutano huo ulilenga kuwajengea uelewa watu wenye ulemavu kuhusu fursa za kiuchumi na changamoto zinazowakabili.

Mshauri wakitaalam masuala ya watu wenye ulemavu Tanzania, Peter Charles Mwita akizungumza kwenye mahojiano na waandishi wa Habari wakati wa mkutano huo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania, Hamadi Abdallah Komboza, alionyesha wasiwasi kuhusu upatikanaji wa ajira kwa watu wenye ulemavu na kutoa wito kwa Kamishna wa Kazi kufanya ukaguzi kwenye mashirika na taasisi zinazopaswa kuajiri watu wenye ulemavu.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania, Jonas Lubalo, alishukuru taasisi ya Ikupa Trust Fund kwa mchango wake katika kusaidia watu wenye ulemavu nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles