27.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

FATMA KARUME ARUSHA KOMBORA, LUGOLA AJIBU

  • Ni kuhusu maagizo yake kwa IGP Sirro
  • Ofisa adai mbwa Hobby yupo Kurasini

NA AZIZA MASOUD – DAR ES SALAAM


SIKU moja baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola,  kumpa saa kadhaa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, kumpatia taarifa za mahali alipo mbwa maalumu wa polisi Kikosi cha Bandari anayefahamika kwa jina la Hobby, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Fatma Karume, amesema  Waziri huyo hana mamlaka ya kumwamrisha Mkuu huyo wa Polisi.

Ukiacha agizo hilo, alilolitoa juzi jioni baada ya kufanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam, akitaka awe amepatiwa maelezo hayo ifikapo Alhamisi saa 12:00, kabla ya hapo, siku mbili zilizopita Waziri huyo alimtaka IGP Sirro ampe maelezo ya magari kutotembea usiku na maduka kufungwa saa 12 jioni kwa kuhofia majambazi.

Akizungumzia uamuzi huo wa Lugola, Fatma, ambaye alianza kwa kuandika ujumbe kupitia akaunti yake ya Twitter, kabla ya kuzungumza na MTANZANIA Jumamosi, alisema Waziri hawezi kumwamuru Mkuu wa Polisi kwa kuwa hana mamlaka naye kisheria.

“Hivi vyeo kama vya Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Majeshi huwa vinajitegemea, ndiyo maana wanateuliwa na Rais, ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu, hizi taasisi zimeundwa kipekee kwa mujibu wa Katiba yetu, Waziri hawezi kumwamrisha kiongozi anayeteuliwa na Amiri Jeshi Mkuu, yeye anapaswa kutoa ushauri tu kwa Amiri Jeshi Mkuu,” alisema Fatma.

Alisema kulingana na Katiba na sheria za nchi, yapo mamlaka anayopewa waziri kwa watu  anaowaongoza, na kwa kuzingatia mamlaka hayo, zipo taasisi ambazo mawaziri wana mamlaka nazo.

Alizitaja taasisi hizo kuwa ni pamoja na Shirika la Umeme  nchini (Tanesco), ambalo lipo chini ya Waziri wa Nishati,  ambaye anatajwa kuwa na mamlaka kamili kisheria.

Katika hilo, alisema sheria ya uundwaji wa Tanesco inampa mamlaka Waziri wa Nishati kumwamrisha mkurugenzi wa shirika hilo kufanya jambo fulani, kwakuwa ana mamlaka naye.

“Nadhani unaona tofauti, yupo waziri mwenye mamlaka na yupo anayepaswa kushauri, kwa sababu hiyo, sasa ujumbe wangu kwa mawaziri hawa ni kwamba wakianza kuvitumikia vyeo vyao wawe wanauliza kwa watu ambao ni wazoefu wizarani ili wajue mamlaka na mipaka yao inapoishia na si kukurupuka,” alisema Fatma.

Kabla hajazungumza na MTANZANIA Jumamosi, Fatma aliandika ujumbe kupitia kwenye akaunti yake ya Twitter akikosoa baadhi ya uamuzi wa Lugola, kama unavyosomeka hapa chini:

“Cheo cha IGP anakipata kwa sababu anaqualify (anakidhi vigezo) kuwa IGP, appointment (uteuzi) inafanywa na Rais. Commander in Chief (Amiri Jeshi Mkuu) ni Rais na si Waziri. Waziri anamshauri au anashauriana na IGP. Hawezi kumwamuru IGP. Commander wa IGP ni Rais peke yake na si Waziri”.

Ni kauli hizo za Fatma pamoja na mambo mengine, ndizo zililielekeza gazeti hili kumtafuta Waziri Lugola kwa njia ya simu.

Akijibu hoja ya kutokuwa na mamlaka ya kumwamuru IGP, Lugola alisisitiza kuwa, anayo ya kumwagiza, isipokuwa yale ya kumfukuza kazi.

“Mimi ni Waziri wa Mambo ya Ndani, hawa wote ni timu yangu, hivi vyombo vyote vipo chini yangu, ndiyo maana hata juzi juzi uliona nimemfukuza mtu kwenye kikao baada ya kuchelewa, hayo mamlaka ninayo, ndiyo maana ya Waziri wa Mambo ya Ndani, sasa walitaka wale mbwa nikamuulize nani kama siyo Sirro?” alihoji.

Inaendelea………………….. Jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

 

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles