29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, October 2, 2022

SERIKALI KUTOA BOTI TATU KUBEBEA WAGONJWA VISIWANI

Na Mwandishi Wetu – Kigoma

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepanga kupeleka boti tatu zinazokwenda kasi ili kubebea wagonjwa kwenda hospitali za rufaa katika vijiji vinavyozungwa na maji.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema hayo leo Ijumaa Julai 20, wakati wa ziara yake katika kijiji cha Mwamgongo mkoani Kigoma.

“Kutokana na kilio cha Wanamwamgongo tutajipanga kuleta boti tatu hasa kwa wajawazito katika vijiji vinavyozungukwa na Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Visiwa vya Mafia,” amesema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema mbali na boti hiyo ataleta gari mpya ya kubebea wagonjwa mara baada ya ujenzi wa barabara inayotoka Kigoma mjini kwenda katika Kijiji cha Mwamgongo.

Kwa upande wake Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba amesema: “Waziri Ummy ameonesha uhai katika Kijiji cha Mwamgongo kwani ujio wake utafanya wanawake na watoto kupona na ameandika historia nyingine ya kuwa  kiongozi wa pili wa kitaifa kuja hapa baada ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1968,” amesema Serukamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,474FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles