Bashiri Na Meridianbet Mahali Popote, Muda Wowote!
Miongoni mwa mifumo ya usafiri inayopatikana nchini Tanzania, pikipiki almaarufu kama bodaboda ni kinara kwenye sekta ya usafiri hasa maeneo ya mijini na vijijini. Hili ni kundi ambalo, pengine limetoa ajira kwa vijana wengi nchini Tanzania na, kwa kujiajiri kwao kunaongeza pato lao binafsi na Taifa kwa ujumla. Meridianbet tunaamini katika ubingwa. Kwetu, maana halisi ya ubingwa ni uwezo wa kila mmoja kufanya kazi kwa juhudi ikiwa ni pamoja na kushikana mikono kwa kadiri inavyowezekana.
Kwa maana hii ya ubingwa, Meridianbet imewafikia madereva bodaboda katika vituo mbali mbali vya usafiri huo jijini Dar es Salaam. Safari hii, kampuni ya Meridianbet iliwatembelea madereva wa vituo vya wilaya ya Temeke na Kinondoni. Pamoja na mengi yaliyowafikisha Meridianbet kwenye vituo hivi ni Pamoja na suala zima la kusisitiza umuhimu wa kufuata sheria za barabarani.
Madereva Pamoja na wanaotembea kwa miguu, wote kwa Pamoja ni watumiaji wa barabara. Wanapokua barabarani wote wanategemeana hasa katika suala la usalama. Kwa misingi hii, Meridianbet kwa kushirikiana na uongozi wa kituo cha polisi Temeke, waliwafikia madereva bodaboda wilayani humo na kuwa elimu ya usalama barabarani.
Pamoja na kuwapatia elimu hiyo, Meridianbet ilitoa vifaa muhimu kwa madereva bodaboda wanapokuwa katika shughuli zao za usafirishaji. Miongoni mwake, zilitolewa kofia ngumu (helmets) pamoja na vizibao maalumu (reflectors) ambavyo vinamsaidia dereva wa bodaboda kuonekana hata anapokuwa mbali. Hivi ni vifaa muhimu kwa madereva ambapo, wanasisitizwa kuvitumia muda wote wanapokuwa katika majukumu yao. Hili haliishii kwa madereva tu, bali pia, wanasisitizwa kuhakikisha abiria wanaowahudumia pia wanakua salama kwa kuvaa kofia ngumu (helmets) muda wote wanapokuwa safarini.
Akizungumza katika tukio hili, mmoja wa mabalozi wa Meridianbet, Bwana Jacob Mbuya, aliwakumbusha madereva bodaboda kusimamia kanuni na taratibu zilizowekwa na mamlaka za usalama nchini ili kuweza kufanya kazi katika mazingira salama kwao na vifaa vyao. Aidha, Bwana Jacob aliwaasha madereva bodaboda ambao pia wengi wao wanafurahia huduma za kubashiri na Meridianbet kuhakikisha wanabashiri kistaarabu bila kujiingiza kwenye matumizi mabaya ya vipato vyao ambayo yatapekea kushindwa kuendesha Maisha yao na familia zao.
Miongoni mwa madereva bodaboda walionufaika na ujio wa Meridianbet kituoni kwao (hawakupenda majina yao kutajwa), wameishukuru kampuni ya Meridianbet Pamoja na polisi waliowatembelea kwenye kituo chao na kuwapa elimu ya usalama barabarani. Pia, madereva hao (kwa kipekee) wameishukuru Meridianbet kwa kuwapatia vifaa muhimu zaidi katika shughuli zao za kila siku na kuiomba kampuni hiyo kuendesha matukio kama haya mara kwa mara na kuwafikia madereva bodaboda waliowengi zaidi nchini.
Safiri Salama Ukiwa na Meridianbet!