27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Simbachawene aongoza kikao cha kujadili utekelezaji wa Anwani za makazi

Na Mwandihi Wetu, Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene ameongoza kikao cha Mawaziri kwa lengo la kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za makazi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.

Kikao hicho kimefanyika Mei 27, 2022 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dodoma ambapo kilihudhuriwa na mawaziri wakiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa, Waziri wa Nchi Ofisi wa Makamu wa pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Hamza Hassan Juma na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula.

Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akichangia hoja wakati wa kikao cha mawaziri cha kujadili taarifa utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi katika kikao cha Mawaziri kilichofanyika Mei 27, 2022 Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dodoma.

Kikao hicho kimefanyika kama sehemu ya maandalizi ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 2022 nchini ambapo itakuwa Sensa ya Sita tangu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 na sensa ya watu na makzi hufanyika kila baada ya miaka 10.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles