24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ubalozi wa Tanzania wafanya kongamano la Utalii, Uwekezaji Ghana

Na Mwandishi Maalumu
-Accra,Ghana

Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Nigeria, Wenye Uwakilishi Sambamba nchini Ghana, umefanya Kongamano la Utalii, Uwekezaji na Biashara (Tanzania-Ghana Tourism, Investment and Trade Forum (TG-TITF), Mei 28, 2022, kwa kufanya Forum ya Utalii, Uwekezaji na Biashara (Tanzania-Ghana Tourism, Investment and Trade Forum (TG-TITF), jijini Accra, Ghana.

Jukwaa hilo lilikusudi kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania Bara na Zanzibar, fursa na vivutio vya uwekezaji pamoja fursa za biashara. Jukwaa hilo liimefunguliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, ambapo pia limehudhuriwa na wadau wa sekta hizo kama vile Jumuiya za Wafanyabiashara, Wenyeviwanda, Kilimo na Madini za Ghana, Makampuni ya Utalii, Wafanyabiashara na Wawekezamitaji.

Katika kongamano hilo mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wenyeviwanda, na Madini ya Ghana, Clement Osei-Amoako.

Aidha, Taasisi za Jamhuri ya Muungano, hususani TTB, TIC, ZIPA, EPZA, TanTRADE, Jumuiya za Wafanyabiashara, Wenyeviwanda, Kilimo na Madini za Tanzania Bara na Zanzibar, zilishiriki na kuelezea kwa undani fursa, miundo, majukumu na nafasi zake katika kukuza Biashara, Utalii na Uwekezaji nchini Tanzania.

Pamoja na mambo Mengine, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria anbaye pia anawakilisha nchi ya Ghana, Dk. Benson Bana, alieleza kuwa Jukwaa hilo linakusudia kuleta taasisi, jumuiya za wafanyabiashara, wawekezaji wa Tanzania na Ghana kuona namna ya kushirikiana na kukuza mahusiano ya uwili baina ya nchi hizi, ambazo uhusiano wake ulianzatangu kipindi cha waasisi wa mataifa haya, Mwl. Julius Nyerere na Kwame Nkrumah, Marais na Baba wa Mataifa ya Tanzania na Ghana mtawalia.

Aidha, juhudi hizi ni kuunga mkono Juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan, katika kukuza sekta ya Utalii hasa kupitia Filamu ya “The Tanzania Royal Tour”.

Kwa Upande wake Balozi Mstaafu wa Ghana nchini Ufaransa, Genevieve Delali Tsegah, Balozi Mstaafu wa Jamhuri ya Ghana nchini Ufaransa, alipongeza hatua hiyo na kusema kuwa itakwenda kufungua milango ya utalii na uwekezaji nchini Tanzania kutokana na kazi kubwa inayofanywa na viongozi wake

Naye Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kwaku Group, Dk. Ken Kwaku, ambaye pia ni Balozi wa Heshima nchini Tanzania,

Mkurugenzi na Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Utalii ya Ghana aliyewakilishwa na Alfred Asumadu Naibu Mkurugenzi wa Masoko pamoja na Alisa Osei-Asamoah, Rais wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii Ghana (Tour Operators Union of Ghana), Dk. Sarah Marjie, Mhadhili Mwandamizi, Chuo Kikuu Cha Ghana Lego, na Mratibu wa masomo ya Lugha ya Kiswahili waliwasilisha salaam na kuchangia katika Mada mbalimbali.

Aidha, Jukwaa hilo lilihudhuriwa na baadhi ya Watanzania waishio nchini Ghana. Wanafunzi wa Lugha ya Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Ghana Legon walishiriki na kuhudumia jukwaa hilo ili kuwa karibu na Tanzania ambako Lugha ya Kiswahili ilizaliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles