23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Familia ya Leticia Nyerere kutoa tamko Ijumaa

leticia nyerereNA KOKU DAVID, DAR ES SALAAM

FAMILIA ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Leticia Nyerere, imesema baada ya kukamilisha majadiliano inatarajia kutoa tamko la kifamilia Januari mosi.

Akizungumza na MTANZANIA jijini Dar es Salaam, msemaji wa familia ya Msobi Mageni, John Shibuda, alisema kwa sasa haina cha kuzungumza na kwamba baada ya kukaa ndipo itakuwa na neno la kusema.

Alisema mgonjwa bado yupo hospitali na kwamba familia ndiyo itakayoamua kuhusu nini kifanyike au hatua gani ichukuliwe.

“Kwa sasa familia haina chochote cha kuongea kuhusu mgonjwa, lakini baada ya kukutana kama familia tunatarajia kutoa neno siku ya Ijumaa,” alisema Shibuda.

Hata alipoulizwa kuhusu hali ya mgonjwa huyo, alikataa kusema na kusisitiza kuwa taarifa zote zitatolewa Ijumaa.

Mbunge huyo ambaye Julai 27 mwaka huu alitanganza kuhama Chadema na kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM) amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Doctors Community iliyopo Maryland nchini Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles