28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

Nyalandu: Msaidieni Profesa Maghembe

nyalanduNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

“Watendaji ni kiungo muhimu kwa waziri kutekeleza majukumu yake, ni matumaini yangu mtampa ushirikiano katika hili,” alisema.

Nyalandu alisema ushirikiano huo utawezesha rasilimali za nchi kama misitu na wanyama kuendelea kuwapo na kutumika kwa njia endelevu.

Alisema umuhimu wa wizara kuendelea kutangaza vivutio vya utalii ili kuhakikisha malengo katika sekta hiyo unazidi kufikiwa.

 

“Wizara hii ina watendaji wema na wanaojitolea kutimiza majukumu yao, kuna askari wa wanyamapori na misitu wanaofanya kazi kwa weledi,” alisema Nyalandu.

Kwa upande wake, Waziri Maghembe alisema wizara yake imejipanga kufanya kazi kwa kasi zaidi na kuendeleza yale ambayo yalifanywa na mtangulizi wake.

“Ninatambua mwenzangu alifanya kazi kubwa ya  kuendeleza na kusimamia wizara… na mimi kwa kushirikiana na watendaji tutafanya kazi na kuzidi kuleta mafanikio,” alisema Profesa Maghembe.

Alitaja baadhi ya maeneo yatakayopewa kipaumbele ni kukomesha wizi wa magogo na vita dhidi ya ujangili wa wanyama pori.

“Watu walikuwa wanavuna magogo na kujifanya kama yanatoka nchi jirani ya Zambia, ulipambana na kutengeneza ushirikiano na nchi hizo…tutaiga mfano wako,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles