TENDO la ndo ni kitu muhimu ndani ya uhusiano. Kukosekana kwa tendo hili ndani ya ndoa kunaweza kusababisha mtafaruku baina ya wapendanao.
Leo ningependa kuzungumzia sababu za msingi kwa nini watu waliofikia umri unaoruhusiwa kukutana kimwili kuhakikisha wanafanya hivyo.
1. Hupunguza mawazo
Tendo la ndoa husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongo wa mawazo. Pia huufanya mwili kutengeneza homoni zinazosaidia kupunguza msongo wa mawazo. Wanasayansi wanathibitisha kuwa wapenzi ambao uhusiano wao hauko vizuri, huwa hawafanyi tendo hili kama inavyotakiwa.
2. Huziweka homoni za mwanamke katika uwiano sawa
Tendo hili linafaida nyingi kwa wanawake, si tu kumfanya awe mwenye furaha bali pia humsaidia katika kuzalisha homoni ya estrogen ambayo humsaidia kuogeza muda na uwezo wa kubeba mimba. Pia husaidia katika mzunguko wa hedhi. Faida hizi zinaweza kuonekana iwapo utafanya tendo la ndoa angalau mara moja kwa wiki.
3. Hupungaza hatari ya kupata saratani
Hupunguza mwezekano wa kupata saratani ya titi kwa wanawake na saratani ya tezi dume kwa wanaume.
4. Husaidia mtu kuishi maisha marefu
Hupunguza uwezo wa mtu kupata magojwa kwa kuogeza kinga ya mwili na kumfanya asizeeke haraka.
5. Kuimarisha misuli
Husaidia kuimarisha misuli ya mwili mzima na hivyo kumfanya mwanamke/mwanamume kuwa na mwonekano mzuri (shape). Pia husaidia misuli ya nyonga kuwa imara na hivyo kumwepusha asijikojolee ovyo.
6. Hupunguza maumivu
Maumivu ya kichwa cha kawaida tu isiwe sababu ya wewe kuto fanya tendo la ndoa kwa kuwa inaweza kuwa ni dawa ya kutuliza maumivu.
7. Kukufanya utake zaidi kila wakati
Jinsi unavyozidi kufanya tendo la ndoa, ndivyo unavyozidi kutamani zaidi. Hali hii inaweza kumuogezea mwanamume nguvu za kiume.
8. Husaidia kupunguza uke na nguvu za kiume
Kufanya tendo la ndoa husaidia kuimarisha misuli ya nyonga, ambapo ikiwa imara inaweza kusaidia uke wa mwanamke kubana.
9. Husaidia kupata usigizi
Kama unatatizo la kupata usingizi, ni muda mwafaka sasa kwako kufanya tendo la ndoa. Hii itakusaidia kupata usingizi wa kotosha. Kufika kileleni husababisha kutoka kwa kemikali inayosaidia mwili kutulia.
10. Huleta muonekano mzuri
Utafiti unaonesha kwamba wanawake ambao hufanya tendo la ndoa mara kwa mara huwa wenye furaha na kuwa na mwonekano mzuri kuliko wale wasiofanya tendo hilo.
11. Huweka mzunguko mzuri wa hedhi
Jinsi mwanamke anavyozidi kufika kileleni ndivyo hedhi zake hukaa vizuri na damu kuwa chache. Pia hupunguza maumivu kipindi cha hedhi.
12. Husaidia wapenzi kujuana zaidi
Kufanya tendo la ndoa husaidia kumfurahisha mweza wako na kujua vitu gani anapenda, hali hii inaweza kukufanya ukamjua vizuri mwenza wako zaidi ya mama au baba yake mzazi.
13. Hupunguza uzito
Ukifanya tendo la ndoa angalau mara mbili kwa wiki inaweza kukusaidia kupunguza uzito wa mwili.
14. Hufanya ngozi kuwa nyororo  Â
Kama unangozi mbaya, kufanya tendo la ndoa kunaweza kukusaidia ngozi yako kuwa nyororo.
15. Huimarisha ubongo
Tendo la ndoa huogeza kiasi cha damu ambacho kinakwenda kwenye ubongo na hivyo kukufanya kuwa makini zaidi.