30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Faida 15 za tendo la ndoa

0e91efa4ee3e2bb2_shutterstock_340210601

TENDO la ndo ni kitu muhimu ndani ya uhusiano. Kukosekana kwa tendo hili ndani ya ndoa kunaweza kusababisha mtafaruku baina ya wapendanao.

Leo ningependa kuzungumzia sababu za msingi kwa nini watu waliofikia umri unaoruhusiwa kukutana kimwili kuhakikisha wanafanya hivyo.

1. Hupunguza mawazo

 

Tendo la ndoa husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongo wa mawazo. Pia huufanya mwili kutengeneza homoni zinazosaidia kupunguza msongo wa mawazo. Wanasayansi wanathibitisha kuwa wapenzi ambao uhusiano wao hauko vizuri, huwa hawafanyi tendo hili kama inavyotakiwa.

2. Huziweka homoni za mwanamke katika uwiano sawa

 

Tendo hili linafaida nyingi kwa wanawake, si tu kumfanya awe mwenye furaha bali pia humsaidia katika kuzalisha homoni ya estrogen ambayo humsaidia kuogeza muda na  uwezo wa kubeba mimba. Pia husaidia katika mzunguko wa hedhi. Faida hizi zinaweza kuonekana iwapo utafanya tendo la ndoa angalau mara moja kwa wiki.

3. Hupungaza hatari ya kupata saratani

 

Hupunguza mwezekano wa kupata saratani ya titi kwa wanawake na saratani ya tezi dume kwa wanaume.

4. Husaidia mtu kuishi maisha marefu

 

Hupunguza uwezo wa mtu kupata magojwa kwa kuogeza kinga ya mwili na kumfanya asizeeke haraka.

5. Kuimarisha misuli

 

Husaidia kuimarisha misuli ya mwili mzima na hivyo kumfanya mwanamke/mwanamume kuwa na mwonekano mzuri (shape). Pia husaidia misuli ya nyonga kuwa imara na hivyo kumwepusha asijikojolee ovyo.

6. Hupunguza maumivu

 

Maumivu ya kichwa cha kawaida tu isiwe sababu ya wewe kuto fanya tendo la ndoa kwa kuwa inaweza kuwa ni dawa ya kutuliza maumivu.

7. Kukufanya utake zaidi kila wakati

 

Jinsi unavyozidi kufanya tendo la ndoa, ndivyo unavyozidi kutamani zaidi. Hali hii inaweza kumuogezea mwanamume nguvu za kiume.

8. Husaidia kupunguza uke na nguvu za kiume

 

Kufanya tendo la ndoa husaidia kuimarisha misuli ya nyonga, ambapo ikiwa imara inaweza kusaidia uke wa mwanamke kubana.

9. Husaidia kupata usigizi

 

Kama unatatizo la kupata usingizi, ni muda mwafaka sasa kwako kufanya tendo la ndoa. Hii itakusaidia kupata usingizi wa kotosha. Kufika kileleni husababisha kutoka kwa kemikali inayosaidia mwili kutulia.

10. Huleta muonekano mzuri

 

Utafiti unaonesha kwamba wanawake ambao hufanya tendo la ndoa mara kwa mara huwa wenye furaha na kuwa na mwonekano mzuri kuliko wale wasiofanya tendo hilo.

11. Huweka mzunguko mzuri wa hedhi

 

Jinsi mwanamke anavyozidi kufika kileleni ndivyo hedhi zake hukaa vizuri na damu kuwa chache. Pia hupunguza maumivu kipindi cha hedhi.

12. Husaidia wapenzi kujuana zaidi

 

Kufanya tendo la ndoa husaidia kumfurahisha mweza wako na kujua vitu gani anapenda, hali hii inaweza kukufanya ukamjua vizuri mwenza wako zaidi ya mama au baba yake mzazi.

13. Hupunguza uzito

 

Ukifanya tendo la ndoa angalau mara mbili kwa wiki inaweza kukusaidia kupunguza uzito wa mwili.

14. Hufanya ngozi kuwa nyororo   

 

Kama unangozi mbaya, kufanya tendo la ndoa kunaweza kukusaidia ngozi yako kuwa nyororo.

15. Huimarisha ubongo

 

Tendo la ndoa huogeza kiasi cha damu ambacho kinakwenda kwenye ubongo na hivyo kukufanya kuwa makini zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles