30 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Zifahamu aina kuu tatu za mazoezi, faida zake – 2

GYM

MAZOEZI YA KUNYANYUA VITU VIZITO

WIKI iliyopita nilisema kuwa kuwa mazoezi haya ni kama kupiga push-ups, kubeba vyuma na kutumia mashine maalumu kunyanyua au kusukuma uzito. Hutumia nguvu kubwa hivyo ni vigumu kuyafanya kwa muda mrefu bila kupumzika.

Kwa kuwa sehemu kubwa ya kichocheo kinachotumika wakati wa mazoezi ya aina hii ni sukari, si mafuta—aina hii ya mazoezi haihitaji hewa ya oksijeni. Ni mazoezi muhimu katika kuimarisha misuli na mifupa. Pia huchangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza kiasi cha homoni muhimu kama vile testosterone mwilini. Mazoezi haya pia huufanya mwili utumie sukari na mafuta kwa muda mrefu hata baada ya kusita kufanya mazoezi. Mara nyingi sukari ndiyo hutumika wakati wa mazoezi na mafuta huanza kutumika baada ya mazoezi kuisha. Hivyo, ni muhimu pia katika kupunguza uzito na kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu. Inashauriwa kufanya mazoezi haya angalau mara mbili mpaka tatu kwa wiki.

MUHIMU:

Miili yetu hupoteza kiasi cha misuli kadri umri unavyosogea, kitu ambacho huanza tunapokuwa na umri wa miaka 30. Mifupa yetu pia huanza kukosa nguvu. Kwa kuwa mazoezi ya aina hii huimarisha nguvu ya misuli na mifupa, kufanya mazoezi ya kunyanyua na kusukuma uzito ni muhimu  kwa watu wenye umri mkubwa. Inashauriwa kufanya mazoezi yanayohusisha misuli mikubwa kama vile ya mapaja na kifua.

KUNYOOSHA NA KULAINISHA VIUNGO

Mazoezi haya ni kama yoga, kufanya stretch ups, na kunyoosha misuli. Aina hii ya mazoezi ni muhimu katika kuviweka viungo kama vile magoti katika hali nzuri ya kujongea. Pia husaidia kunyoosha misuli baada ya kuwa katika hali ya kutanuka. Misuli hutanuka wakati wa mazoezi au mtu anapokuwa katika mkao fulani kwa muda mrefu. Kwa maana hiyo, ni muhimu kufanya mazoezi haya kabla au baada ya kufanya aina nyingine ya mazoezi. Inashauriwa kufanya mazoezi haya mara kwa mara, ikiwezekana zaidi ya mara moja kwa siku. Kwa mfano, inashauriwa kujinyoosha kila baada ya saa moja endapo mtu atakuwa kwenye shughuli ya kuketi kwa muda mrefu.

MUHIMU: Usikae mfululizo kwa zaidi ya saa moja bila kusimama na kutembea kidogo, au kujinyoosha. Kwa kufanya hivi kutakusaidia kujikinga na magonjwa kama maumivu sugu ya mgongo.

UJUMBE WA KWENDA NAO

Hakikisha unafanya aina zote za mazoezi kila wiki. Kila zoezi lina faida zake na huwezi kupata faida zote kwa kufanya aina moja tu ya mazoezi.

Kama unataka kufahamu zaidi, wasiliana nami kwa barua pepe [email protected]

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles