NEW YORK, Marekani
KAMPUNI inayomiliki mtandao wa kijamii wa Facebook imebadili jina na sasa itaitwa Meta, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya maboresho ya nembo yake.
Aidha, mabadiliko hayo hayatamaanisha kuwa jina ‘Facebook’ kutoonekana kwenye simu za watumiaji, bali kampuni hiyo inayomiliki pia mitandao ya Instagram na Whatsapp ndiyo itakayoitwa Meta.
Hatua hiyo inakuja baada ya kashfa nyingi dhidi ya Facebook baada ya watumishi wake wa zamani kuvujisha nyaraka za siri za kampuni hiyo.
Miaka sita iliyopita, kampuni ya Google nayo ilibadili jina na kujiita Alphabet lakini jina hilo limeshindwa kujenga umaarufu kwa watumiaji wengi wa mitandao.