23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi wasaidieni vijana watimize ndoto zao – Ryoba

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wazazi na walezi wametakiwa kuwajibika kwa kuwatimizia watoto mahitaji yao ya msingi ili kuhakikisha wanasoma bila vikwazo na kutimiza ndoto zao.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Wahenga Aluminium, John Ryoba, ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya 12 ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Ari iliyopo Wilaya ya Ilala.

Amesema wazazi na walezi wana mchango mkubwa katika mafanikio ya watoto na kuwataka watimize wajibu wao hasa kwa wanafunzi wanaotarajia kufanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne.

Wahitimu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Ari wakicheza wakati wa mahafali yao.

Aidha amewaasa wahitimu ambao watakosa nafasi ya kuendelea na masomo kutokata tamaa badala yake wakuze vipaji vingine walivyonavyo.

“Kesho ya mtu inatengenezwa na Mwenyezi Mungu na wewe mwenyewe ukijiamini hivyo, haimaanishi ambao hawatafanikiwa ndiyo wamefeli maisha, wanaweza kujaribu vipaji vyao,” amesema Ryoba.

Mkurugenzi huyo pia ameahidi kushirikiana na wadau wengine kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo.

Naye Mkuu wa shule hiyo Flora Msonge, amesema wanajivunia kuongezeka kwa walimu wa sayansi na kujengwa kwa maabara za sayansi hatua iliyoondoa changamoto za ujifunzaji kwa wanafunzi wanaopenda masomo ya sayansi.

Hata hivyo amesema wana changamoto za kukosekana kwa uzio na kusababisha jamii inaoishi jirani pamoja na mifugo kuingia eneo la shule, uchakavu wa mashine ya kudurufu maandishi, uchakavu wa kisima na pampu ya kusukuma maji pamoja na ukosefu wa viti na meza za walimu.

Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake Kaka wa shule hiyo, Brian Masawe, amesema; “Kwa muda wote tuliokaa shuleni tumefanikiwa kupata elimu bora kutoka kwa walimu wetu itakayotusaidia kupambana na changamoto mbalimbali katika jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles