33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

EWURA yafafanua mabadiliko bei ya mafuta

ewura2Na Jonas Mushi, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetoa ufafanuzi wa jinsi inavyobadilisha bei za   mafuta kwa kuzingatia bei za soko la dunia baada ya kuwapo malalamiko mbalimbali kuhusiana na suala hilo.

Mkurungenzi wa EWURA, Felix Ngamlagosi alisema jana kuwa yamekuwapo madai kwamba mamlaka hiyo inachelewa kushusha bei za nishati hiyo ili ipate faida kubwa na kwamba haishushi bei kwa kiwango kilichoshuka katika soko la dunia.

Alisema lazima watu watambue kuwa kushuka kwa bei ya mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia kunachangia kushuka kwa bei katika soko la ndani kwa asilimia 46 hadi 49 na si kwa uwiano wa asilimia 100 kama watu wanavyodhani.

Ngamlagosi alisema hiyo inatokana na gharama zinazoambatana na uingizaji wa mafuta kama vile gharama za usafirishaji, faida za waagizaji mafuta, kodi za Serikali, gharama za bandari na tozo za mamlaka mbalimbali.

Alisema kuna tofauti kati ya bei za mafuta ghafi na mafuta yaliyosafishwa.

“Bei za mafuta katika soko la ndani hukokotolewa kwa kutumia gharama halisi za uagizaji mafuta nchini ambazo hutokana na meli za mafuta yaliyopokelewa katika  mwezi husika, ambayo huwa yamenunuliwa mwezi uliotangulia,” alisema

Hivi karibuni EWURA ilitangaza kushuka bei ya mafuta ambako bei ya petroli ilishuka toka kiwango cha juu zaidi,   Septemba 2014 cha Sh 2,267 kwa lita kufikia Sh 1,898 kwa lita  Januari 2016.

Bei ya dizeli ilishuka toka kiwango cha juu zaidi  Aprili 2014 cha  Sh 2,149 kufikia Sh1,747 kwa lita   Januari 2016, na bei ya mafuta ya taa ilishuka toka kiwango cha juu zaidi  Februari 2014 cha Sh 2,069 kufikia Sh 1,699 kwa lita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles