29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

EU kufanya mazungumzo ya kibiashara na Marekani

Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zimekubaliana kuanza majadiliano rasmi ya kibiashara na Marekani.

Hatua hiyo inakuja katikati mwa kitisho kutoka kwa Rais Donald Trump ya kuongeza ushuru katika bidhaa za shirika la Umoja wa Ulaya la Airbus.

Umoja wa Ulaya kwa hivi sasa uko katika mvutano wa kibiashara na Marekani, huku rais Trump akitishia kuongeza ushuru kwa magari na bidhaa nyingine za Ulaya.

Ufaransa ambayo ilikuwa ikijaribu kusogeza mbele mazungumzo hayo ya kibiashara hadi baada ya uchaguzi wa Umoja wa Ulaya, ilipiga kura kupinga hatua hiyo, wakati Ubelgiji ikijizuia kupiga kura.

Msingi wa mazungumzo ya Tume ya Ulaya ni pamoja na kupunguza ushuru wa bidhaa za viwanda na kuifanya iwe rahisi kwa makampuni kuonyesha bidhaa zinazofikia viwango vya Umoja wa Ulaya na Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles